Kitengo cha maafa kianze kutoa msaada wa counselling kwa mashuhuda wa ajali kubwa

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Kuna ajali mtu akishuhudia zinaweza kumuathiri kisaikolojia, just imagine katika ajali ya juzi mtu ushuhudie live watu wakiungua moto hadi kufa, au kujua tu watu kadhaa ndugu na marafiki wameungua kwa moto, ile Trauma ile shock inaweza kukuandama kwa muda mrefu sana katika maisha yako.

Lakini pia kuna wanaonusurika, hawa ni rahisi kwa akili pia kuwaruka kidogo kwa sababu ya msongo wa mawazo kutokana na kuchungulia kifo au kutokana na kumbukumbu ya mateso waliyopitia.

Kwa hiyo natoa rai kwa Kitengo cha maafa kianze kutoa councelling bure kwa waathirika wa ajali kubwa au ajali za kutisha.

Namna hii tutasaidia kupunguza saddism, psychological trauma, dipression .k

Kitengo cha maafa chini ya ofisi ya Waziri mkuu, pelekeni wanasaikolojia morogoro wakawatibu wananchi walioshuhudia ile ajali

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom