Kitendo cha Andrew Chenge kutaka kurudi Bungeni ni kiashiria kuwa Mwenyekiti wa CCM 2020 aliwalazimisha wapishe wengine?

Wasalaam Members!

Tangia nisikie Mh Chenge amechukua form ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimejikuta nikitafakari sana kuhusu kutokurudi kwake Bungeni 2020 na hizi mbio zasasa za Uspika.

Mwaka 2020 kwenye kura za maoni Mh Andrew Chenge alishinda japokuwa jina lake lilikatwa kwemye kamati kuu hivo halikurudi kwaajili ya kugombea Ubunge na hakuonesha kama anashida na ilo.

Sasa kajitosa kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la JMT rasmi na habari zilizopo huyu mwamba anaenda kuchukua icho kiti, swali Je! Hayati Magufuli alimlazimisha astafu siasa? Bado Mh Chenge alitakani kuendelea kuwa Bungeni?
Anakwenda kuondosha sheria zote za kifalafala zilizotungwa na Magufuli na Ndugai
 
Yule bwana alikuwa anatengeneza utawala wa ki syndicate
yani pamoja na kukiunga JF bado ujakuwa na akili za kutosha kuwa Magu ndio alikuwa anajitahidi kuzivunja hizo syndicate ila kwa sasa ndio zinaludi kumalizia pale walipoachia.
 
..Ni kwasababu ana uwezo mkubwa ktk masuala ya sheria na taratibu za bunge kuliko wana-ccm wengi mle bungeni.

..hujawahi kusikia kwamba ktk bunge maalum la katiba, ccm ilikuwa inamtegemea Chenge ktk kuandika katiba pendekezwa?

..zaidi, alipokalia kiti cha mwenyekiti wa bunge, Chenge aliongoza vikao kwa busara na weledi kuliko wenyeviti wengine.

..unaweza kumchukia Chenge kwasababu ya tuhuma za ufisadi lakini ukweli utabaki kuwa ana uwezo mkubwa na uzoefu kuhusu masuala ya bunge na taratibu zake.
Kwa nafasi kama hiyo hupaswa hata kutuhumiwa
Hivi
Mgao wa escrow
Kuweka uchawi bungeni kuoitia camera za bunge nazo ni thuma kweli za uongo kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..vijana wako active ktk ngono hivyo wana uwezekano mkubwa wa kuathirika na ukimwi. Kwasababu hiyo hawastahili nafasi za uongozi.

..hoja ya vijana vs wazee haina tija sana. Tuangalie uwezo wa mgombea.

Nani amekwambia wazee hawapo active kwenye ngono ? Hao ndio wapo active na 100% wameungua kwa sababu hawapo makini na kinga
 
Nani amekwambia wazee hawapo active kwenye ngono ? Hao ndio wapo active na 100% wameungua kwa sababu hawapo makini na kinga

..ndio maana nimekwamba hoja ya vijana vs wazee haina tija.

..ngoja nikupe mfano mmoja. Mwaka 2015 Januari Makamba, Zitto Kabwe, walikuwa na hoja yao ya Raisi kijana.

..Sasa hivi umri umewatupa huwasikii tena wakitetea hoja ya vijana kuongoza.

..Wacha wagombea wote wajitokeze, na kusiwepo ubaguzi wa umri,jinsia,dini, kabila,au rangi.
 
Hatutaki watu wa kwenda kusinzia bungeni kwa faida ya Nchi .
 
Hatutaki watu wa kwenda kusinzia bungeni kwa faida ya Nchi .

..kama mijadala inayoendelea ni ya kijinga kwanini mbunge apoteze muda kusikiliza.

..ningekuwa bungeni halafu wanapewa nafasi kuchangia ni Msukuma,Kibajaji, Kingu, Polepole,.. ningeutumia muda huo kusinzia.
 
..ndio maana nimekwamba hoja ya vijana vs wazee haina tija.

..ngoja nikupe mfano mmoja. Mwaka 2015 Januari Makamba, Zitto Kabwe, walikuwa na hoja yao ya Raisi kijana.

..Sasa hivi umri umewatupa huwasikii tena wakitetea hoja ya vijana kuongoza.

..Wacha wagombea wote wajitokeze, na kusiwepo ubaguzi wa umri,jinsia,dini, kabila,au rangi.
Vijana wamepewa nafasi nyingi sana, hakuna walichokifanya tukadhani ni tofauti na wazee
Hivi vijana si akina Makonda, Sabaya, Happi , Polepole n.k.

Nani anaweza kunyoosha kidole na kusema kijana yule ni tofauti. Tena wamepwaya kiasi kwamba tunawasikiliza akina Mzee Warioba kila siku.

Hoja ya vijana au wanawake haina maana! mwenye uwezo apewe nafasi aongoze hata kama ana miaka 15 au 95.
 
Uzoefu wake utumike kama mshauli kwa watu wenye nguvu na Nchi kwa ujumla yeye apumzike awaachie vijana

Hatutaki speaker atakaekua anaenda India kutibiwa kila siku kwa kodi za watanzania kwa umri alionao
Suala la kuumwa hilo usiliseme wapo waliowaona wenzao wagonjwa matokeo yake wameugua wao na kufa na wamewaacha waliodhaniwa wana hali mbaya.
 
Back
Top Bottom