Napita tu, ila nimeona niwaachie kaushauri kadogo.
Najua kwamba watu wengi uchukulia kama sifa kuwa na likitanda likubwa sana bed room, 6*6 au 6*5, Lakini kiukweli haya mavitanda makubwa ni moja ya kichocheo cha kupanua kutoelewana ndani ya ndoa hasa kunapokuwa na mkwaruzano kidogo.
Hii inasababishwa na kuwapo kwa opportunity ya kulala bila kugusana usiku kucha sababu kila mtu anaweza akachagua kulala mwisho kabisa kiasi kwamba hata ujiviringishe vipi ukiwa usingizini huwezi kumgusa mwenzio, hivyo nashauri wanandoa wenzangu tu opt vitanda vidogo vidogo ambavyo ukipanda tu kitandani adui huyu hapa tayari, labda akimbilie kulala chini.
Alamsiki.