Kitabu Bora cha Simulizi 2019

Chilojnr

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
308
Reaction score
1,354


Vijana watatu, Robinson, Richard na Robert wanapanga kuingiza kiasi cha Dola za Kimarekani, Bilioni nne ambazo ni zaidi ya Shilingi trilioni kumi. Ili kuingiza pesa hizo, wanahitaji akili kubwa, kupambana usiku na mchana mpaka kuhakikisha kiasi hicho cha pesa kinaingia kwenye akaunti zao.

Robinson mwenye uwezo wa kuchezea kompyuta anatakiwa kuutumia kufanikisha kiasi hicho cha pesa kinaingia, Robert mwenye uwezo wa kuchora mbinu mbalimbali anatakiwa kuitumia akili yake kuhakikisha pesa hizo zinaingia kwenye akaunti zao na hata Richard, kutokana na uzuri wa sura aliokuwanao, anatakiwa kuutumia ipasavyo kuhakikisha pesa hizo zinaingia kwenye akaunti zao.

Vijana hao wanaingia mchezoni, wanapanga kuanza kwa msichana Natasha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya hapo wahamie nchini Kenya, wapige pesa kwa rais, jaji na chama cha upinzani, wakimaliza waelekee nchini Marekani, iwe isiwe ilikuwa ni lazima pesa hizo zipigwe haraka iwezekanavyo.

Ila kabla ya yote, wanatakiwa kuanza kumsomesha kijana aitwaye Vonso nchini Marekani ili siku wakipelekwa mahakamani, mtu huyo awaokoe kupitia sheria, na walimtaka asome sana kitu ambacho kijana huyo aliahidi kukifanya.

Kukipata kitabu hiki ni shilingi 10,000 kwa Dar, unaletewa na sh. 15,000 mikoani, unatumiwa. Wasiliana nami kwa namba 0763986156.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…