Nyie ndo mnataka na kufuta kiingereza kwenye rasimu,bado nasema kiswahili hatufiki kokote sb hatuna pesa pia hatuna utaalam wowote.Vipi Mfananisho wako kati ya Nchi ya Kenya na Angola ambapo wananchi wa Angola hawajui Kiingereza kabisa na wanajua Kireno badala yake, Je, hapo unasemaje maana yake Kiuchumi Angola wapo mbali sana!
Je vipi kuhusu Kenya na Uganda mbona haujafananisha hapo? Na Je Uganda Na Tanzania?
Kwa kifupi ni kwamba wewe Kenya haupajui vizuri, kwa taarifa yako wananchi wengi wa Kenya kwa mfano Nairobi zaidi ya 70% hajui lugha yoyote kwa 100% yaani hawawezi kuongea kilugha chao vizuri, hawawezi kiingereza vizuri na pia hawawezi Kiswahili vizuri matokeo yake wamekuja na lugha mpya ambayo ni mseto wa Kiswahili na kiingereza na lugha nyingine waniita ,,sheng'', hivyo nenda Nairobi hata kutembea tu na usifikia kwa wadosi nenda uswazi ambako ndiko zaidi ya 70% ya Watu wa Nairobi wanaishi!
Hivyo kwa Maswala ya Lugha TZ tuko mbali sana si ajabu ktk Kusini mwa jangwa la Sahara tunaongoza Afrika!
Nyie ndo mnataka na kufuta kiingereza kwenye rasimu,bado nasema kiswahili hatufiki kokote sb hatuna pesa pia hatuna utaalam wowote.
Ndugu zangu watz nimefikia uamuzi wa kuona kuwa lugha ya kiswahili ni mojawapo ya sababisho la umaskini wetu.Mwezi December nilifanya utafiti wa kupima utajiri wa kuongea lugha ya Kiswahili,Kiingereza, na Lugha ya asili ya mama yake(Native language)kati ya mwanafunzi wa std 4 wa TZ na std 4 wa Kenya.Matokeo ni kuwa Mtanzania hakuweza kuongea kwa ufasaha hizo lugha tatu,Mkenya aliweza kuongea kwa ufasaha kabisa lugha zote tatu.Katika kiswaahili Mtanzania alikuwa anaweka 'R' penye 'L' na kinyume chake pia alikuwa anatumia maneno mengi yasio fasaha,Kiingereza hakuweza kutengeneza sentensi ya kumwomba maji mama yake na hakuweza kuongea lugha ya asili yake kabisa!.Hii ilikuwa tofauti sana na Mkenya ambaye aliweza kuongea kiswahili na kiingereza kwa ufasaha mkubwa pia aliweza kuongea lugha ya mama yake ya kiluo vizuri na kiluhya.
Rasimu ya katiba ililiona hilo hivyo kuweka lugha za taifa kuwa kiswahili na kiingereza.Hii ingefanya masomo yote isipokuwa kiswahili kufundishwa kwa kiingereza na hivyo kufanya kizazi hicho cha kitanzania kuongea kiingereza kwa ufasaha wakiwa bado primary school.Kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati za bunge la katiba;wajumbe walio wengi wameondoa kiingereza na kuacha kiswahili kitumike kama lugha rasmi ya serikali lakini wajue wanazidi kuwatenga watanzania.Kenya wamefanya kiswahili na kiingereza ziwe lugha za taifa lakini kuanzia bush school(chekechea) ni kiingereza isipokuwa soma la kiswahili.Hii inatufanya tusiweze kujiamini na kuwa "maimuna".Sasa angalieni mapendekezo hovyo za hizi kamati za BMK ya walio wengi!.
Kiingereza ndio lugha kuu ya kitaalam na kibiashara ulimwenguni hivi.Hivyo ni vizuri tufanye watu wetu waweze kuongea kiingereza kwa kufanya kiingereza kufundishwa kuanzia chekechea masomo yote isipokuwa kiswahili tu.Yes we can.
Hebu fikiria itakuwa raha namna gani sokoni,kwenye dala dala,uswahilini,kule manerumango kwa binti kinyogoli ni these,this,what,how are you?,thank you,welcome!.:flame:
Huyu jamaa badala ya kusema yeye ni masikini anataka kulazimisha wengine wote tuwe kama yeye. Haiwezekani!Si Ujibu kwanza nilichokuuliza? Kama hauna Jibu sema tu!
Mi ni mtu mzima. Nilianza kujifunza Kiingereza nilipofikia darasa la tatu zama hizo. Nadhani ilikuwa vema kabisa nianze literacy katika lugha iliyokuwa karibu nami zaidi kabla sijaanza lugha za kigeni. Nilipofika sekondari kulikuwa na kipindi kifupi cha adjustment. Lakini baada ya hapo nimeweza kujifunza Kiingereza kwa kiwango kizuri tu kwa kiwango cha kitaalamu kabisa.
Mwanzilishi wa thread hii, unajaribu kufanya maoni yako kuwa facts au kitu kinachotokana na utafiti wako. Kwa mfano, wataalamu waliochunguza juu ya lugha za mafunzo ya awali watakuambia unalolidai la kuanza na lugha ya kigeni ni wazo ambalo si zuri kwa makuzi ya elimu ya watoto. Pia, kama ilivyo katika mfano wangu mwenyewe huo, kuanza kujifunza lugha ya kigeni baadae zaidi si chanzo cha kutokujifunza Kiingereza vizuri. Mimi na wale tuliosoma wakati wetu tulijifunza Kiingereza vizuri tu.
Kama utaangalia mifumo ya elimu ya nchi mbalimbali za ulaya utaona wanakisema sana Kiingereza. Lakini hawaanzi elimu yao na Kiingereza. Lakin wanapoanza kujifunza lugha za kigeni wanazifundisha vizuri pamoja na resources zinazotakiwa.
Wazo la kuabudu Kiingereza kiasi cha kuona kwamba lugha nyingine hazifai hapa duniani NDILO hasa wazo la kimaskini. Umaskini wa mawazo. Tunatakiwa kujifunza lugha nyingi na kupata umahiri wa hali ya juu. Kila lugha ina mambo muhimu. Stop this self-hatred.