Kisomo kirumirumi.


Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,603
Likes
1,003
Points
280
Idd Ninga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2012
2,603 1,003 280
*KISOMO KIRUMIRUMI.*
1)wimbo sasa wanifunza,na vyema nauelewa.
Ndo kwanza tumeshaanza,wala hatujachelewa.
So kila zazi la nyanza,lakili kulewalewa.
Kisomo kirumi rumi,chaundwali tukisome.

2)nyumba inatoa funza,.na viza yapasuliwa.
Donda lapakwa uvinza,wale wanyanyapaliwa.
Mtetemo toka mwanza,ndo mwanzo unacheua.
Kisomo kirumi rumi,chaundwali tukisome.

3)kichini chini walia,kusema kwa ogopewa.
Mikatazo wajitia,wasije kutimuliwa.
Huzuni aigizia,asijeye kusemewa.
Kisomo kirumi rumi,chaundwali tukisome.

4)mitusi kuvumilia,si ajabu umekuwa.
Hilo nalo ogopea,kama hujalielewa.
Kua ukivumilia,jana ulivyolelewa.
Kisomo kirumi rumi,chaundwali tukisome.

5)wimbo unafurahisha,ule uliotungiwa.
Mwenyewe wajichekesha,wao watafurahiwa.
Japo hawezi wafisha,ndi hivyo ushachelewa.
Kisomo kirumi rumi,chaundwali tukisome.

Shairi=KISOMO KIRUMI RUMI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga na mashairi.
 

Forum statistics

Threads 1,237,144
Members 475,462
Posts 29,279,439