Ni kijana mwenzangu sekta ya afya, mwaka huu mwanzoni aliamua kwenda kutoa posa kwa binti ambaye alipanga aanzishe naye familia. Binti mwajiriwa wa serikali na asili yao ni kanda ya ziwa ila wanaishi na familia katika moja mikoa wa Pwani. Mshenga alitumwa pamoja na baadhi ya wanafamilia wa...
Mrejesho wa Thread hapo juu
Baada ya vuta ni kuvute kati ya familia ya kijana na binti kuhusu mahari.
Wanafamilia wa kijana wengi walionyesha kuchukizwa na tabia ya familia ya binti, baadhi ya wanafamilia wakiapa kuwa kama kijana akiendelea na mipango ya kumuoa huyo binti, wao hawatashiriki kabisa katika jambo hilo.
Kutokana na hali hiyo ya kutofikia muafaka kijana akakubali bora yaishe, Mshenga akatuma barua kwa familia ya binti kuwa kwa mahari hiyo ya milioni 5 bila kupungua , wao wameshindwa.
Baada ya wiki familia ya binti ikarudisha barau ya posa juu imeandikwa na wino mwekundu, IMEKATALIWA pamoja na shilingi laki tano za kishika uchumba.
Baada ya hayo ndugu wa kijana wengi wameonyesha kufurahishwa na muafaka huo.
Kijana amekubali matokeo kuwa haikuwa ridhiki yake.
Binti yeye ameonyesha kukubali kishingo upande kwani hii ni posa ya pili imekataliwa nyumbani kwao dhidi yake.