Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 4,188
- 9,165
KISA CHA SIMBA WA ALLAH (SWT)
Wahshi bin Harb muuaji wa Simba wa Mwenyezi Mungu ambaye ni Hamza bin Abdulmtwalib (ra) ambaye ni ammi yake Mtume(saw) na ndugu wa Mtume(saw) kwa kunyonya. hebu endelea kusoma hapa...
Katikati ya vita vya Uhud, alikuwepo mwanamume mmoja aliyekuwa akivizia kimya kimya, akiwa ameshika mkuki usiojua huruma. Macho yake yalielekezwa kwa shabaha moja tu: Hamza bin Abdul-Muttalib, Simba wa Mwenyezi Mungu na mpendwa wa Mtume Muhammad(saw) kuliko wote.
Mkuki mmoja tu... na kiongozi wa mashahidi akaanguka shahidi.
Na muuaji alikuwa: Wahshi bin Harb.
Alifanya hivyo kwa ajili ya uhuru wake... lakini hakujua kuwa mkuki huo utamchoma Mtume(saw) moyoni, na kumbukumbu hiyo ingemwandama maisha yake yote.
Miaka ikapita, Mtume akaingia Makkah kama mshindi(katika fat'hu Makkah).
Watu wakawa wanazungumza maneno ya chinichini:
“Sasa Muhammad ameingua Makkah je atamlipizia kisasi cha ami yake? atamuua Wahshi...”
Lakini Mtume hakuwa kama watu wengine... alimwacha huru!
Alimwambia tu:
“Jifiche usinione.”
Naam, hakuweza kumtazama usoni lakini hakulipiza kisasi.
Wahshi aliendelea kuishi akiwa mfungwa wa majuto...
Aliamka kila siku akiwa na huzuni ya dhambi, na kulala akiwa na aibu ya kile alichokifanya.
Kila mara aliinua mikono yake kumuomba Allah amkubalie toba na ampatie fursa ya kuufanyia jambo Uislamu.
Na Allah, aliyemrehemu zaidi ya nafsi yake, alimkubalia.
Vilikuja vita vya Yamamah, na akatokea adui mkubwa wa Allah na Mtume Wake: Musailamah al-Kadh-dhaab (muongo).
Hapo ndipo Wahshi alishika mkuki uleule aliomuua nao Hamza, akaelekea vitani.
Mkuki mwingine...
Lakini safari hii uliuangusha uso wa uovu adui mkubwa wa Uislamu.
Baada ya hapo, akasema:
“Nilimuua mtu bora wakati wa ujahili (Hamza), na nikamuua mtu mbaya zaidi katika Uislamu (ambaye ni Musailamah).”
Ni safari ya ajabu kutoka kwenye shimo la majuto hadi kilele cha ushindi na fahari.
Hadithi ya Wahshi inatufundisha jambo moja tu:
👉🏼Mlango wa toba haujafungwa na Allah haangalii yaliyopita yetu ikiwa tumesadiki na kutubu kwa dhati katika makosa yetu.
Ukiishamaliza kusoma, leo ni Usiku wa Mtume Muhammad(saw) mswalie Mtukufu wa Mitume na kipenzi chetu Mtume Muhammad(saw).
“Allahumma salli ‘ala Muhammad wa ‘ala aalihi wa swahbihi ajma’in.”
🔹Kwa hadithi zaidi, jiunge nasi katika ukurasa wetu wa Sufian Mzimbiri