Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,563
- 7,321
Leo hii kalamu yangu itapaa na kusafiri hadi mbali, katika bara la Ulaya kusini mashariki. Kuitafuta nchi ya Ugiriki ambapo nitasafiri kilomita 9329.2 kwa muda wa masaa 126 hadi kufika kwenye nchi hii kubwa ya kihistoria na utajiri mkubwa wa hadithi na visa vya ajabu sana.
Mji mkuu wa Ugiriki, Athens-umepambwa kwa hekaya za kale na hadithi tamu sana kuzisoma.
Kalamu ya Kabati ikifika kwenye maktaba za kale za mji huu, itakutana na hadithi za miungu Zeus, Apollo, Athena, Poseidon,Hermes ,Hera na wengine wengi.
Itakutana na hadithi za mashujaa wa kale kina Hercules na kina Perseus na hata zile za majitu ya kutisha kama mbwa mwenye vichwa vitatu Cerberus. Au lile joka la majini lenye vichwa visivyofikwa na umauti, Hydra.
Hawa wote tutawasoma humu kwenye chaneli yetu. Ombi letu ni lilelile, kuwaleta ndugu na jamaa zenu wanaopenda fasihi kujumuika nasi.
Hadithi ni nyingi sana lakini leo hii, nimepata bahati sana ya kufungua kurasa za vitabu vya kale kuhusu
Twe’nzetu.
Medusa ni nani?
Medusa ni jina lenye asili ya kigiriki, kumaanisha “ulinzi au usalama”.
Hadithi na simulizi zinammulika kama mmoja kati ya wanawake warembo sana na waaminifu kuwahi kupumua katika ardhi ya Ugiriki ya kale yaani “Ancient Greece”.
Alikuwa ni mtoto wa kike katika familia ya dada watatu waliozaliwa kwa wazazi ,Phorcys na Ceto. Dada zake walikuwa ni wawili walioitwa, Sthenno na Euryale. Ambapo kwa pamoja watatu hawa walijulikana kama “The Gorgons”. Dada watatu waliokuwa viumbe wa kutisha, japo Medusa alikuwa mrembo kuliko dada zake.
Naomba niweke mambo sawa hapa. Sio kwamba Medusa alizaliwa ni kiumbe wa kutisha bali dada zake ndio walizaliwa hivyo wakiwa wanatisha, yeye alizaliwa kama mwanadamu kamili na sio kamili tu bali mrembo sana sanaaa.
Lakini baadaye yalimkuta masaibu yaliyomfanya ashike njia na kufata asili ya dada zake wawili, na kwa pamoja wakaunda hiki kikundi cha “The three gorgons”. Ni nini kilimkuta Medusa?
Ni nini kilimkuta Medusa?
Medusa alikuwa binti mrembo mtulivu, mwenye soni na bikra. Alipendelea sana kuwa mfanya kazi na mtawa wa hekalu. Hekalu la mungu Athena, muungu wa kike wa kigiriki aliyesimamia busara, vita na sanaa. Medusa alijitolea kuwa mtumishi kwa mungu huyu, akawa mtumishi wake.
Kwa desturi hakuna jambo jema linalokosa ubaya ndani yake. Hii ndio asili ya ulimwengu, lenye ubaya lina uzuri na lenye uzuri lina ubaya ndani yake. Urembo wa binti Medusa, ukawavutia wanaume wengi sana…wanadamu hata miungu. Akatokea mungu mkuu wa bahari, Poseidon akampenda sana Medusa.
mungu Poseidon akaanza kuuza lugha yake kwa Medusa. Lakini Medusa akamkatalia. Alikuwa tayari ameshajiweka wakfu kuwa mtumishi bikra na muaminifu kwa mungu wa kike Athena. Wanaume hatukati tamaa. Poseidon akatembea na ule msemo wa mkate hauwi mgumu mbele ya chai.
Lakini safari hii msemo ukamsaliti huu mkate ulikuwa umekandwa kwa jiwe, hakuna chai yoyote ile ingeweza kuufanya laini. Akakasirika.
Ikatokea ile siku ya tarehe, ilionifanya hata mimi nikuandikie wewe usome. Poseidon akaibuka kutoka baharini, upendo ulimzidia ukageuka kuwa tamaa; akamkimbiza Medusa akitaka kumpata kwa nguvu.
Maneno yake hayakutosha kumshawishi, sasa alitaka kutumia misuli yake.
Naam,
Safari hii alitaka kulisaga jiwe kwa nguvu zake mwenyewe, hakuitaji msaada wa chai.
Medusa alikimbilia kwenye hekalu la mungu Athena kuomba msaada. Lakini ilikuwa kazi bure, hakusikilizwa!
Poseidon akamkamata Medusa na akambaka palepale katika hekalu la mungu Athena. Hakujali juu ya utakatifu au usafi wa hekalu. Jamaa akamaliza matamanio yake na akaondoka! Tatizo likaanzia hapo.
Laana ya mungu Athena kwa Medusa,
Maswali ni mengi sana…kuwa ni kwa nini huyu mungu aliyekuwa akiabudiwa na kutukuzwa sana na Medusa hakutokea kumsaidia? Je alikuwa amelala? Au alisafiri labda…hebu fikiria.
Majibu ni mengi sana, wapo waliohitimisha kuwa na yeye alikuwa akimuonea wivu Medusa kwa sifa za urembo wake. Na wengine wakasema kuwa alikuwa ni mjivuni sana.
Lakini baada ya mungu Athena kugundua kuwa amri ya sita imevunjwa hekaluni mwake tena kwenye sakafu yake, sakafu ya nyumba yake; akakasirika sanaa.
Akamchukia Medusa na akamtupia laana mbaya mno.
Kuwa kila unywele mmoja wa kichwa chake ugeuke na kuwa nyoka, awe na sura mbaya kiasi kwamba kila anayemtazama ageuke na kuwa jiwe. Alipoona kuwa bado laana aliyompa ni nyepesi mno , huyu mungu akamuongezea na mkia wa nyoka dada yetu Medusa. Hebu pumzika sekunde kadhaa ufikirie.
Ule uzuri wa uso wake ulioyaburudisha macho ya watu, leo hii unawafanya wawe mawe. Inasemekana alikuwa mbaya sana.
Kutokana na madhara ya ubaya na kutisha kwa sura yake, ilimbidi Medusa ajitenge na ulimwengu wa binadamu wa kawaida. Akawatafuta wale dada zake na kujichimbia kwenye chimbo la wabaya wa sura, mbali huko mapangoni. Kutoka kuwa mtumishi mrembo wa hekalu mpaka kuwa hayawani anayejificha mapangoni. Hakika alilaaniwa akalaanika.
Je Medusa ni muovu?
Filamu nyingi, maonyesho na hadithi za kimapokeo zinamuonyesha Medusa kama kiumbe wa kutisha sana mwenye kuua watu na kudhuru umma wa watu. Hata ukitazama picha zake baadhi anaonyeshwa kama kiumbe mwenye laana na roho chafu mwenye kuadhibu na kuua watu.
Lakini sivyo!
Mwanzo alikuwa mwema na muadilifu lakini laana aliyoipata ndiyo iliyomuharibia wajihi wake. Aliwaumiza wengi waliomtazama wakageuka kuwa mawe, akatengwa na ulimwengu.
Yeye ni muhanga wa unyanyasaji na uonevu aliofanyiwa na Poseidon pamoja na Athena. Hakupenda kuwa hivi, ni umbile lake tu lilibadilishwa. Akatengwa!
Alipobakwa na Poseidon alipata ujauzito wa watoto wawili mapacha, lakini asingeweza kuwazaa.
Ilimbidi afe kwanza ndio hawa watoto wazaliwe. Walikuwa ni Chrysaor aliyekuwa binadamu wa kawaida, na Pegasus aliyekuwa farasi mzuri mwenye mabawa.
Picha zao nitazileta humu mzitazame.
Mwisho wa Medusa ulikuwaje?
Binadamu ni viumbe wanaotegemea sana fursa. Fursa ni popote na katika hali yoyote ile hata katika hatari. Basi licha ya maafa aliyokuwa akiyasababisha Medusa, bado kuna watu waliona kuwa atakuwa na faida sana. Hawa wakahitaji kichwa chake! Kwao huku kutisha kwa Medusa, kulikuwa ni fursa!
Walikitafuta na kukiwinda kwa hali na mali, walishindwa wengi sana wakageuka mawe. Kile kichwa chake kilichotisha ndicho walikihitaji.
Maana kingetumika kama silaha ya kupambaa na maadui walioshindikana. Kumbuka kuwa kama ungekitazama tu, ungeogopa na kugeuka kuwa jiwe.
Walishindwa wengi, isipokuwa mmoja tu, aliyeitwa Perseus. Huyu alipata ushauri na msaada kutoka kwa miungu na kafanikiwa kukikata kichwa cha Medusa.
Zipo hadithi zinazosimulia kuwa alipambana naye kwanza akitumia kioo na nyingine zinasimulia kuwa alimvizia akiwa amelala, akatumia taswira yake kwenye kioo na kumkata kichwa, akamuua.
Inasimuliwa kuwa baada ya kufa kwa Medusa, wakazaliwa hawa ndugu wawili Chrysaor na Pegasus. Wakati huo dada wawili wa Medusa walikuwa wametoka, waliporudi na kukuta maafa haya wakaanza kumfatilia huyu muuaji Perseus bila mafanikio.
Huu ndio ulikuwa mwisho wa Medusa.
Medusa katika dhahania mbalimbali,
Inasemekana kuwa huyu Perseus alikitumia kichwa cha Medusa kama silaha njiani mwake, na dhahania zinasema alikutana na jitu njiani kaskazini mwa Afrika, lilioitwa ATLAS. Akaliomba hifadhi likamkatalia likapigana naye, akaliadhibu kw akulionyesha kichwa cha Medusa. Likageuka mlima mkubwa wa mawe. Leo hii tunauita mlima wa Atlas. Sio maneno yangu ila ni hadithi za kimapokeo!
Tena wanasema huko huko kaskazini, huyu Perseus alipita kwenye kanda za Libya, damu ya Medusa ikawa inatiririka njiani. Hii damu ikageuka kuwa nyoka wengi wakali sana na wenye sumu kali. Ndio maana hadi leo Afrika, ndio bara lenye nyoka hatari zaidi duniani. Sio mimi jamani. Ni dhahania za mapokeo!
Matokeo ya simulizi ya Medusa katika ulimwengu wa sasa,
Medusa ina maana ya “ulinzi” kama tulivyoona hapo mwanzo. Leo hii simulzi ya Medusa imekuwa kama ngao ya kutetea haki za wanawake wanaozalilishwa na kunyanyaswa na jamii. Imechochea sana kuwapa kipaumbele wanawake kuishi kwa uhuru, kiasi kwamba nembo ya kichw acha Medusa kinatumika kwa dhumuni hili.
Mapambo mengi na ngao za Ugiriki, zina nembo ya kichwa cha Medusa ikiashiria alama ya ulinzi na usalama. Kama ambavyo kichwa chake kiliweza kugeuza watu waovu waliotaka kumuua na kuwa mawe.
Nembo ya kichwa cha Medusa imetumika pia katika fasheni za mavazi mbalimbali pia.
Unaifahamu kampuni ya VERSACE? Ile nembo ya kichwa cha mwanamke ile…itazame vyema. Ni Medusa huyo. Aliyevumbua hiyo aliitwa Gianni Versace, alisema kuwa Medusa alikuwa mrembo sana kiasi kwamba kila aliyemtazama hakuweza kuacha kumtazama. Nguvu ya ukike, “female power”!
Zipo filamu zimeigizwa zenye Medusa ndani yake, kama muhusika pia.
Katazame…filamu ya CLASH OF TITANS ya mwaka 2010. Pia filamu ya PERCY JACKSON AND THE OLYMPIANS ya mwaka 2010 pia.
Wewe mwanafasihi ulikuwa na ufahamu gani juu ya Medusa, dada mwenye sura mbaya na nyoka wengi kama nywele kichwani?

MEDUSA, mwanamke mwenye sura mbaya ya kutisha na kichwa chenye nywele-nyoka. Ambaye simulizi ya kisa chake haijawa ya kusisimua tu, bali imeleta mapinduzi katika maisha yetu ya leo.Twe’nzetu.