Kisa cha kweli cha Mama aliyelia kwa msiba wa mwanae kiasi cha kumkufuru Mungu. Ni somo kwetu sote.

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Nilikutana na huyu mama mtu mzima wa miaka zaidi ya 75, aliyefiwa na mwanae pekee aliyekuwa anamjali sana.

Alikuwa na wanawe wengine watatu ambao kiukweli walionekana ni mzigo kwake, kwani walikuwa walevi na wasio na msaada kwa mama huyu zaidi ya hata wakati mwingine kumwibia au kumpora kile kidogo alichokua nacho ili tu wakapate pombe!

Nakumbuka sana yule alivyokuwa analia kwa uchungu huku akisema "Mungu wangu umemchukua yule aliyenijali na kunitunza ukaniachia mapumbavu!.."
Ilinitia simanzi lakini nikakumbuka mapenzi ya Mungu hayahojowi na mara Zote Mungu hakosei.

Tujifunze kumshukuru Mungu kwa kila jambo!
 
Kilio kinachofanana na hicho kilitolewa na babu yake marehemu mtangazaji Isack Gamba siku ya mazishi yake. Inaumiza sana kuondokewa na mtu uliyempenda sana.
 
Mkuu sasa hapa tunajifunza nini....mana kufiwa na MTU muhimu lazima ulie kwa kila dizaini ila mwisho wa siku unatulia na ishu nyingine zinasonga.......Hakuna kufuru hapa.
 
Back
Top Bottom