Kisa cha Bwana Ugoko na wapangaji wenzie

Kisa cha Bwana Ugoko na wapangaji wenzie

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,312
Reaction score
12,194
Wapangaji 6 wa nyumba moja mnajichanga na kununua bastola kujihami dhidi ya majambazi. Mnakubaliana kwa kuwa bwana ugoko yuko chumba cha karibu na mlango wa kuingilia basi awe analala na bastola tayari kumkabili yeyote atakayejaribu kuwavamia.

Siku bastola inapowasili toka dukani na kutua mikononi mwa bwana Ugoko, Ugoko anawaamuru wote muweke mikono juu; anawaamuru mgalegale kwenye tope la uani, mruke kichurachura na vitimbi chungu mzima.

Waliowahi kukwaruzana naye huko nyuma na wale anaowadai wanaipata 'fresh'. Halafu, huku mkiwa mmechuchumaa na mikono ikiwa juu, anawasomea marufuku nyingi sana; hairuhusiwi kufungulia radio sauti ikasikika nje, kukaangakaanga ni marufuku na sheria zingine kibao. Akawaapia kuwa yeye si mtu wa mchezo anayetaka na ajaribu aone!.

Baadhi ya majirani wamelalamika chinichini na wengine wamempongeza kuwa Ugoko ni kiboko!.

c&p
 
Wick, post:
Huyu bwana Ugoko namfananisha na Mzee Meko wa mjengo mweupe. Ana roho mbaya kumzidi shetani, anafurahia maumivu ya wengine na kafanikiwa kuwageuza wafuasi wote wa chama cha mataahira (CCM) kua timu ya kumsifu na kumuabudu yeye!
 
Tabia aliyoionesha ndugu ugoko iwe ni fundisho kwa wengine wanaopenda kuwaamini watu kwa kuwapa nyazifa kubwa kushinda uelewa wa wanaempa madaraka hayo.
 
Hata kama huamini uwepo wa Mungu mwisho wa maisha yako utahukumiwa na Mungu mwenye kutoa hukumu ya haki kwa binadamu.
Huyo mjinga state agent kaona aibu mpaka kafuta post yake!... Ni vijingajinga flani vya praise team, vimekosa kazi vinafananisha kila kitu na Mungu!.
 
Wick, post:
Huyu bwana Ugoko namfananisha na Mzee Meko wa mjengo mweupe. Ana roho mbaya kumzidi shetani, anafurahia maumivu ya wengine na kafanikiwa kuwageuza wafuasi wote wa chama cha mataahira (CCM) kua timu ya kumsifu na kumuabudu yeye!
 
Bwana ugoko hataki hata kwenda kutembea anaogopa mtamwibia bastola yake du kazi ipo
 
Sasa ameibadili safari channel nayo inamuonesha yeye tu na kumsifia badala ya wanyama, imekuwa kama vile yeye ni mnyama kivutio cha wageni, sifa zikizidi inakuwa ni aibu
Mkuu kwa hiyo chaneli ya wanyama imegeuja kuonyesha mtu ambaye hayuko ndani ya mapoli yetu ya wanyama?haya ni maajabu ya 8 ya Dunia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom