Kipindi cha Kikwete BASATA ilikuwa inaona kina chura tu?

Ok9

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
4,542
4,117
Kipindi cha JK wengi waliimba wakiuponda utawala wake, tena bila kificho.
Lakini hayo hayakuonekana ni makosa zaidi waliitwa Ikulu (Roma, Mpoto) wakaongee meza 1. Na kwa upande wa BASATA walikuwa hawaoni hilo walikuwa macho kodo kwenye miziki za chura type na ile ya Ney wa Mitego.

Lakini leo mziki wa kumsifia JK hautakiwi. Na ukiangalia huu ulofungiwa ni wa muda mrefu. Ina maana ulikiwa hausikiki?

Wasanii muimbe siasa kama zamani ili kuleta changamoto katka utendaji.
 
Labda wanadhani kumsifia mstaafu, ina maana ya kumponda wa sasa, kitu ambacho si cha kweli!

Kipindi cha BWM, Sugu aliimba wimbo unaoitwa hali halisi, ndani yake alisema " ipo siku tutaandamana mpaka ikulu kwa rais tukamweleze hali halisi", BASATA ya wakati huo ilikuwa na watu wanaojua sanaa na kutambua kuwa mtu anaweza kutekeleza haki yake ya kikatiba ya kutoa maoni kupitia sanaa!

Lakini BASATA ya sasa hivi inacensor too much, inaua creativity, inaua fasihi!!
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Kama mkuu wa mkoa anajiita mungu aliyemchagua unadhani yeye kajiweka kwenye nafasi gani? Asiyepaswa kukosolewa ni Maulana pekee ndiyo maana hata shetani alifukuzwa kwa kutaka kujifananisha na Mola. " mchezo huu haitaki hasira"
 
Yaani hawa BASATA imefikia hatua hawana cha kufanya isipokuwa wanasubiri msanii, atoe kazi halafu wao wacriticize tu!. Wanajustify mshahara wao wanaolipwa kila mwezi!
 
White House ya Wasanii Awamu ya Tano ni Central Police kwa Afande Sirro!
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Awamu hii hutosikia msanii au comedian akimwongelea anko maana anajua ataitwa kwa siro
 
NYIMBO ZIELEKEZWE KWENYE JINSI GANI TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA, NA WENGINE WAJARIBU KUTIA VERSE ZA KUHIMIZA WALE WALIOKUWA WANAISHI KAMA MALAIKA WAISHI KAMA MASHETANI. WALE WAIMBA TAARABU WANYANYUE VIDOLE VYAO HUKU WAKIWASUTA WANAOTAKA MIKUTANO YA HADHARA KIITIO KIWE "mpaka 2020'', WALE WA NGOMA NGUMU WACHANE SANA MISTARI YA KUHIMIZA KUTOKUIJARIBU SERIKALI HII. BONGO FLEVAS BANENI PUA ZENU KWA NYIMBO ZA KUTAJA MAJINA YA WAUZA MADAWA HASA MSISAU YULE MWENYEKITI WA CHAMA KILE CHA MATEJA YULE ANAEVAA MIWANI, YULE JICHO LAKE MOJA SIJUI LILIINGIA VUMBI WAKATI AKIBWIA NANIHII,,,,. SASA OLE WENU MJIDAI MNA MASHAIR MENGINE HAAAAAAAAAAAAAAAA. KAMA NA JOKE HIVI............
 
Tutakomaa nao tuu yan
 
Back
Top Bottom