Kipimo hiki ni cha kweli?

Kipimo hiki ni cha kweli?

ndandawamalenja

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
548
Reaction score
658
Hivi majuzi nilienda kwenye kituo kimoja cha tiba mbadala, pale Mbezi beach. Kinaitwa Fadhaget Sanitarium. Dr. akanipa kidude kidude flani hivi nishike kimeunganishwa na computer, akaclick kinini sijui kikaanza kufanya kama kinascan viungo muhimu vya mwili. Ubongo, moyo, figo, mapafu, etc. Huku kinadisplay activities na information kwenye screen ya laptop. Baada ya dakika 2 hivi kikamaliza na kutoa report. Dr akaanza kunielezea sasa, lakini alichofanya ni kunichanganya tu kwa sababu nikawaza kwamba kile kimachine ni geresha tu. Kwamba kama kupima afya ya mtu ni rahisi hivo, inakuwaje tunapopima mahospitali makubwa kabisa inachukua muda sana, mpaka wakutoe damu kibao na mambo mengine halafu kahospitali kadogo tu kanatechnolojia ya kupima mwili wote kwa sekunde sitini? Hivi hii sio program ya kutuibia ambayo inatoa majibu yaleyale but randomly kutokana na watu mnavyokuja? Naomba wataalam mnifumbue macho!!
 
Hapa ndo mtu unaombwa kutafsiri ndoto, ukitaka kujua ndoto ilikuwaje, unatakiwa uijue na ndoto bila kuambiwa pia!

Kipimo hakina hata jina watu waki Google? Unaambiwa "kidude dude fulani hivi". Hivi huyo Dr. ungemuuliza kipimo hiki kinaitwaje angekuchaji zaidi au?
 
Rudi tena hapo kwenye kituo cha tiba ukaandike jina la hicho kidude halafu ulete hilo jina lake hapa jamvini.
 
dah! maajabu kweli kweli.
anyway nijuavyo mm hata kwenye tafiti device yoyote ile utakayoitumia lazima uitaje na usema kiko calibrated kwa kiwango gani na kimetengenezwa wapi. sasa ndugu yangu mtoa mada kama alitumia stethoscope ama alitumia darubini sisi hatuwez kujua inatakiwa utuambie ni kidude / mashine gani alitumia.
 
jamani jamaa keshawambia aliimwa kwa kutumia kidude sasa nyie mnataka nini tena? just google Kidude na utapata jibu la kifaa alichopimwa nacho...hivi yale ma CT scan ya muhimbili yana kazi gani wajameni?
 
dah! maajabu kweli kweli.
anyway nijuavyo mm hata kwenye tafiti device yoyote ile utakayoitumia lazima uitaje na usema kiko calibrated kwa kiwango gani na kimetengenezwa wapi. sasa ndugu yangu mtoa mada kama alitumia stethoscope ama alitumia darubini sisi hatuwez kujua inatakiwa utuambie ni kidude / mashine gani alitumia.

Yaani my dear gfsonwin siku hizi kumeibuka mambo sijui yanatoka wapi na serikali yetu kimyaaaa! Anchosema mtoa mada ni kama ile wanayoita kupimwa mwili mzima unaambiwa magonjwa kibao in the end wanakwambia dawa tunayo hapa na utaona sio dawa bali unapewa suppliments.... Imesambaa kila mahali watu wanaibiwa pesa zao utakuta mtu ana high blood pressure anaacha dawa za hospitali utamuona siku anakuja na stroke unaambiwa alikuwa anatumia dawa ukisoma zote ni suppliments wanazokuonyesha...
 
Last edited by a moderator:

huu ndio ujinga wetu tena ni kwambie wengi wa wanaotumia hivi vitu ni watu wasomi tu. sijui kwann watu tu wepesi wa hukadaika, utapimwa mwili mzima na kipimo gani?? leo hii watu wanauamaiza vichwa ajili ya discoveriy ya nanodevice kwa ajili ya diagnostics na bado hakijapatikana cha kuweza kupima mwili wote zaid ya MRI labda na CT scan??

watanzania tuache ujinga wa asili na wa kuamini kila kitu bana mambo mengine hayahitaj hata mkono wa serikali bali utash wetu wenyewe tu unatosha. ndio maana wagonjwa wengi wanaokwenda hosp wanakwenda wakiwa at very bad stage kwani muda wote walikuwa wanapaaoteza kwa matatbibu wa kienyeji. poor tanzanians.
 
Jamani mimi nina mtu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la low blood pressure,akapimwa kwenye hospital moja kubwa tu hapa jijini ikaonekana ana tatizo la cholesterol nyingi,akaenda kwa hao jamaa wa tiba mbadala na kuchekiwa kwa hicho kipimo alichokisimulia- ndandawamalenja ikaonekana ana tatizo hilohilo la Cholesterol ila kipimo kiko more detailed kwani kinaonyesha na viwango vya madhara,alipewa dawa ndani ya wiki mbili ile hali ikaondoka kwa almost 50% na ndani ya mwezi akawa fiti sana na alipokwenda kucheck hospital ilionekana hana tatizo tena la cholesterol,pia alipo check na hawa wa tiba mbadala ikaonekana tatizo limeisha,jamaa ana zaidi ya mwaka sasa yuko fiti.-
 
Haya bana/
 
Hivi majuzi nilienda kwenye kituo kimoja cha tiba mbadala, pale Mbezi beach. Kinaitwa Fadhaget Sanitarium. Dr. akanipa kidude kidude flani hivi nishike kimeunganishwa na computer, akaclick kinini sijui kikaanza kufanya kama kinascan viungo muhimu vya mwili. Ubongo, moyo, figo, mapafu, etc. Huku kinadisplay activities na information kwenye screen ya laptop. Baada ya dakika 2 hivi kikamaliza na kutoa report. Dr akaanza kunielezea sasa, lakini alichofanya ni kunichanganya tu kwa sababu nikawaza kwamba kile kimachine ni geresha tu. Kwamba kama kupima afya ya mtu ni rahisi hivo, inakuwaje tunapopima mahospitali makubwa kabisa inachukua muda sana, mpaka wakutoe damu kibao na mambo mengine halafu kahospitali kadogo tu kanatechnolojia ya kupima mwili wote kwa sekunde sitini? Hivi hii sio program ya kutuibia ambayo inatoa majibu yaleyale but randomly kutokana na watu mnavyokuja? Naomba wataalam mnifumbue macho!!
Hili Swali halikupata jibu muafaka, wataala tupeni majibu maana hivisasa hivyo vipimo vimeenea sana. MziziMkavu Kiranga gfsonwin measkron Snipper

http://www.alibaba.com/product-deta...48771402.html?spm=a2700.7724857.29.109.YqvOdm
 
Attachments

  • hausbell-2013-version-medical-de-alta-precision-quantum-magnetic-resonance-body-health-analyzer.jpeg
    hausbell-2013-version-medical-de-alta-precision-quantum-magnetic-resonance-body-health-analyzer.jpeg
    11.9 KB · Views: 176
  • pl1442397-quantum_bio_electric_whole_health_analyzer_for_health_examination_centre.jpg
    pl1442397-quantum_bio_electric_whole_health_analyzer_for_health_examination_centre.jpg
    18.1 KB · Views: 175
  • pl1825017-body_fat_quantum_magnetic_resonance_health_analyzer_portuguese_version.jpg
    pl1825017-body_fat_quantum_magnetic_resonance_health_analyzer_portuguese_version.jpg
    30.7 KB · Views: 185
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom