Kipimo cha muomba kura yoyote tutamuuliza alipambana vipi kuhusu utekaji, Mpina na Gwajima. Hatuna kesi na ninyi sisi kama wananchi.

Kipimo cha muomba kura yoyote tutamuuliza alipambana vipi kuhusu utekaji, Mpina na Gwajima. Hatuna kesi na ninyi sisi kama wananchi.

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
477
Reaction score
1,017
Kwa wanayoangalia haya mambo yanavyokwenda Kuna namna wananchi wameamka na kuelewa kinachoendelea kwaiyo sasa ni rasmi kuwa watanzania si wajinga tena kwenye mambo ya siasa. Wanajua kutofautiasha mbivu na mbichi, nyeupe na nyeusi, uongo na ukweli na hata uje na cheo chochote huna cha kuwadanganya, kwa ilo hongera watanzania kipengele cha ujinga tulishavuka. Juzi tumeshuhudia yaliyotokea kwa Gwajima na Mpina, Yani kusema ukweli na kutaka baadhi ya maswali ya msingi kujibiwa na kushughulikiwa, kinyume chake anaonekana adui ila wanasiasa hasa Wana CCM jueni ya kuwa njia waliochukua ndugu Mpina na Gwajima ndo njia sahihi ya kutengeneza amani na wananchi wenu majimboni. Kila mwenye kihitaji kura atapaswa kujibu swali la wananchi kuwa pamoja na maendeleo mengine katika Jimbo je msimamo wake ulikuwa ni upi katika swala la utekaji na upotevu wa watanzania wenzetu.

Huwezi kuwa mbunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kama huwezi kuisimamia serikali kwa kuhoji juu ya upotevu wa wananchi ambao nyinyi ndo mnataka kuwaongoza.

Na sisi wananchi majimboni swali la kwanza kabla ya salama na kuomba kura itakuwa ni Hilo.

Simama kwenye ukweli atakama itakugharimu kufukuzwa chamani ila historia na jina lako litakumbukwa katika historia ya wapambanaji na siku zote utakuwa na amani kuishi na jamii yako kwakua ukipoteza nafasi kwenye chama bado una nafasi kubwa kwa jamii yako.

Gwajima kaanzisha, Mpina kafuata....who is next.......who is our next hero.....272-2
 
Back
Top Bottom