Kipimo cha kupimia kama nchi imekwea kiuchumi.

Kipimo cha kupimia kama nchi imekwea kiuchumi.

mrregion

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2018
Posts
464
Reaction score
543
Waungwana kila kuchapo huwa najiuliza maswali kadhaa na kukosa majibu sahihi kuwa hivi tunaposema nchi imepanda kiuchumi tunaangalia nini? Je maisha bora kwa mwananchi au ubora wa huduma za jamii au ubora wa miundombinu au kipato cha mwananchi cha kumwezesha kupata huduma za msingi kwa mda na wakati sahihi?

Je kama miundombinu ni bora na wake wake wakawa maskini hapo inakuwaje?

Tanzania ni nchi inayopewa sifa kila siku kuwa tunapanda kiuchumi swali je tumepanda kwenye sekta ipi wakati chanzo cha maarifa elimu ipo nyuma na miundombinu ya elimu ni mibovu?

Muungwana ni vitendo hivyo maneno yasiyo na vitendo hayatoshi kumshawishi mkulima kuwa uchumi umepanda huku hajui soko la mahindi yake liko wapi hadi sasa na wala hajui hatima ya mazao yake wapi atauza na ikumbukwe pembejeo zipo juu kupita maelezo.

Je kigenzo kipi sahihi cha kupima nchi kama Tanzania kuwa imekwea kiuchumi kama hata watumishi tangu mwaka 2015 hawajui nyongeza ya mshahara, na kwa uelewa wangu mdogo wa chuo kikuu ni kwamba kadri ya utafiti mdogo nilionao kuwa kama purchasing power ikiwa kubwa na mzunguko wa hela unakuwa mkubwa ila ikiwa ndogo na mzunguko wa hela unakuwa mdogo.

Naomba majibu kwa anayeelewa na atupe vigenzo vinavyotumika.
 
Watu kumudu Huduma muhimu na serikali tutekeleza miradi kwa fedha za ndani ndio maana ya uchumi kukua. Sisi tunatakiwa mtanzania amudu milo mitatu iliyo bora hayo mengine yafuate
 
Back
Top Bottom