Kipaumbele cha kwanza: Kazi au Familia?

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,147
2,630
Katika jamii yetu, zipo familia (hasa upande wa wazazi) ambazo kazi kwao wanaipa nafasi ya kwanza alafu inafuatia familia, kwao bila kazi familia wanaiona kama vile haijakamilika kwa kila hali.
Na pia zipo familia zingine ndani ya jamii ambazo wazazi katika maisha yao wameipa familia kipaumbele cha kwanza wakiamini ndo njia sahihi ya kuijenga misingi bora ya maisha kwa kizazi chao kwa siku za usoni.

Je, wewe kama mzazi, una maoni gani kuhusiana na hivi vipaumbele viwili, kipi kina faida na kipi kina hasara, waweza toa hata mifano kwa yale uliyojifunza katika mizunguko ya maisha yako polite ulipopitia.

Karibu....
 
Hivi ni vitu viwili tofauti na mfanano wake ni kwenye majukumu ya matumizi ya pesa na muda unaotumika.

Mara zote Familia itakuwa kwanza katika watu unaoishi nao lakini Kazi itakuwa kwanza unapofikiria kuhudumia watu unaowafahamu ( hii ina maana kazi ya kuajiriwa au kujiajiri) hii ni kwa mtazamo wangu.

Mtoa mada hajatufafanulia Familia anayoongelea hapa ni ipi?
Je ni ya mke na watoto? Je ni ya mke , watoto na wazazi wenu? Je ni ukoo??
 
Baba aweke kazi mbele ila akae na familia pia baada ya kazi...

Mama aweke familia mbele ila afanye kazi ndogo ndogo ikiwezekana...
 
..wawili tu mkuu.
Jamani Mungu amesema tuijaze dunia wewe wataka wawili tu? Huoni tutakuwa kinyume na agizo LA Mungu,

Wawili kidogo sana kwani shetan anaangalia hapo Mungu anaangalia hapo sasa kila MTU akiamua kuchukua wake huoni tutaanza upya, tujaribu km 4-6
 
Jamani Mungu amesema tuijaze dunia wewe wataka wawili tu? Huoni tutakuwa kinyume na agizo LA Mungu,

Wawili kidogo sana kwani shetan anaangalia hapo Mungu anaangalia hapo sasa kila MTU akiamua kuchukua wake huoni tutaanza upya, tujaribu km 4-6
Ooops...sita! Una kizazi hicho?
 
Back
Top Bottom