Kiongozi wa upinzani Rwanda, atangaza serikali mbadala

The Certified

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
910
773
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, ametangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo Rwanda, lakini itakayokuwa ikifanya kazi nje ya nchi.

Thomas Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.

Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.

Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Baraza lake la mawaziri
1.jpg
Baadhi ya aliowataja katika baraza lake la mawaziri ni wafungwa wanaotumukia vifungo vya jela nchini Rwanda kwa makosa kama vile kukanusha kuwa mauwaji ya kimbari hayakufanyika nchini Rwanda mwaka 1994.
2.jpg
Bw Nahimana (kushoto) naakiwa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mwaka jana ambapo alizuiwa kwenda Rwanda
Bw Nahimana, ambaye ni mhutu, amelaumiwa kwa kuandika taarifa kadhaa za kikabila na kumkosoa rais Paul Kagame.

Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda.
 
Yale yale ya Uganda
mtu anajiapisha mwenyewe kuwa Rais
mwisho wa siku kimyaa!!
Labda ni serikali mbili za Ufaransa na sio Rwanda
maana zote zitakuwa Ufaransa !!
 
Hai mek sense kabisa, labda hajui maana ya serikali. wangekuwa labda woote wako sehemu moja ningejaribu hata kusema labda ako siriaz.
Bora angeendelea na shughuli zake nyingine tu
 
Hamna inawezekana ukaunda serikali ukiwa uhamishoni na mnajipanga kabisa hapo mnajenga impression kuwa mmejiandaa kuunda serikali mpya ya nchi yenu hivyo mnawapa sababu jeshi na wananchi kuigeuka serikali either kwa maandamano au vita ilimradi itoke madarakani wakijua mbadapa yupo...... hyo techinique imetumiwa sana mbona na wapinzani na wapigania uhuru wengi tu dunia nzima
 
Nipe case moja wapo iliypwahi kutokea mtu katangaza kizembe hivo na aka fanikiwa
 
Mkuuu haihitaji case study kasome tu historia ya world war 2 utakutana na watu walioanzisha serikali nje ya nchi ili kupinga iliyokuwepo kwa mfano spain baada ya Dikteta Franco kuchukua nchi miaka ya 1930 walianzisha yao ikaja kufanikiwa kuchukua madaraka 1977...... hata poland baada ya ujerumani kuweka pandikizi lao walipoivamia nchi hyo 1939 serikali iliundwa kuipinga iliyokuwepo na ilipambana hadi ikaja ikawafurumusha vibaraka waliokuwepo baada ya vita kuisha mwaka 1945 kesi zipo nyingi sana huko czechoslovakia, cjui estoni hayo ma eastern europe countries wlaishakuwa na government-in- exile kibao katafiti utajionea mwenyewe jinsi hii strategic plan works a lot.
 
The nearest years you can relate to that ni 1980s ambayo ilikuwa kipindi cha cold war.
Wale walikuwa hawatangazi tu, lazima uwe na backup ya kimataifa na wakusaidie kweli na wawe na interests hapo.sio unatangaza at your own pleasure kama huyu jamaa
It wont work
 
Mkuu Rwanda wamemchoka huyo bwana sema wamekosa MBADALA maana aliyekuwepo Yule ingabire keshatupwa jela.....so kitendo cha huyu jamaa kuonyesha njia kutawapa sababu ya wanyarwanda hasa wahutu kujiorganize kumpinga huyu dikteta maana wanajua kuna serikali mpya ambayo inaweza kuwavusha kutoka hapo walipo kwenye wimbi la ubaguzi..... it might take years ila trust me mbegu alioipanda huyu na kina nyamwasa ipo siku itazaa matunda.....only time will tell.
 
Back
Top Bottom