Kiongozi tunaye mtaka

Kiongozi tunaye mtaka

Joined
Apr 10, 2014
Posts
8
Reaction score
4
Kumekuwa na kasumba kwa viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kuhama kutoka chama kimoja na kwenda kingine hususani CCM kwenda CHADEMA. Na wengi wakidai kuwa ndani ya CCM hakuna demokrasia ya kweli na pia kukiukwa kwa katiba ya chama hicho.
Kabla ya mchakato wakuwapata wagombea mbalimbali ndani ya chama hicho wanachama hao walisema maneno ya ovyo ya kuviponda vyama vya upinzani. Je swali langu ni kweli kuwa viongozi hawa wamekihama chama cha CCM ili kutukomboa sisi wananchi katika dimbwi hili lililo na takataka za kila aina kama ufisadi, wizi, kufanya mambo kwa kujuana, kutoa tofauti kati ya walionacho na wasionacho na mengine mengi au ni kwa sababu ya kutaka madaraka na kujificha ili wasishughulikiwe baada ya uchanguzi.
Katika nchi hii kuna makundi mawili ambayo ni la WALA NCHI ambao ni wachache na WANANCHI ambao ndio kundi la wengi na walio wengi hawana maamuzi sahihi. Basi mwaka huu 2015 wanacnhi tunatakiwa kutoa maamuzi sahihi ili kuonyesha nini watanzania tunataka katika nchi hii, kiongozi tumchague kwa sababu tunaamini atatuletea maendeleo na si kwa sababu ya fedha zake.
 
Back
Top Bottom