Kiongozi Muadhamu: Marekani inaeneza propaganda za kuifanya Iran iogopwe

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,174
10,650
4bk4332aa9c06e6or7_620C350.jpg


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, hatua ya Wamarekani ya kung'ang'ania kuiwekea vikwazo mbalimbali Iran ni njama za kueneza chuki na kulifanya taifa hili liogopwe na kwamba, kivitendo hatua hiyo imekuwa kikwazo katika ushirikiano wa kiuchumi wa nchi hii na mataifa mengine.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika hadhara ya maelfu ya wafanyakazi wa pembe mbalimbali za Iran kwa mnasaba wa Wiki ya Wafanyakazi na kubainisha kwamba, ukwamishaji mambo wa Wamarekani katika muamala wa kibenki ni mfano wa wazi kabisa katika uwanja wa mtazamo mbaya wa Iran kwa Marekani na kuongeza kuwa, sababu ya mabenki makubwa duniani kutokuwa tayari kushirikiana na Iran ni anga ya kuifanya Iran iogopwe iliyoletwa na inayoendelea kudumishwa na Wamarekani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria matamshi ya viongozi wa Marekani ya kudumisha vikwazo dhidi ya Iran na kuongeza kuwa, viongozi hao wanadai kwamba, Iran ni nchi ambayo imekuwa ikiunga mkono ugaidi na huenda ikawekewa vikwazo kutokana na hilo na ujumbe wa maneno hayo ni kutaka nchi nyingine zisishirikiane na Iran na natija ya hilo ni kuingiwa na hofu na woga benki na wawakezaji wa kigeni wa kushirikiana na Iran.

Ayatullah Khamenei amebainisha kwamba, Wamarekani wanadai kuwa, sababu ya mataifa ya kigeni kutoshirikiana na Iran ni hali ya ndani ya taifa hili katika hali ambayo kwa sasa katika Mashariki ya Kati hakuna nchi yenye amani na usalama kama Iran. Kuhusiana na suala la ugaidi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Wamarekani ndio magaidi wabaya zaidi na kwa mujibu wa ripoti zilizopo wangali wanaunga mkono makundi ya kigaidi.
 
Iran ni taifa linalofadhili ugaidi duniani ndio maana Saudia kawawekea ngumu hijja mwaka huu.
 
Iran ni taifa linalofadhili ugaidi duniani ndio maana Saudia kawawekea ngumu hijja mwaka huu.
Kinyume chake ndio sahihi, Osama ni muiran au msaudi? waliotekeleza ugaidi wa 9/11 ni 15 kati 19 ni wasaudi, alqaeda, isis wote ni sunni wenye mrengo wa kiwahabi unaofadhiliwa na Saudia, hakuna hata muiran hata mmoja alieshiriki katika ugaidi mkubwa na Iran haijavamia nchi nyingine yoyote kwa kipindi cha miaka 200
 
Mungu barik taifa la kiislam la iran....na mataifa yote ya kiislam.

''hawawezi kuwa radhi nanyi mpaka mfuate mila zao''........

Mataifa yote yanayoua watu ovyo Mungu hawezi kuwabariki bali atawabanika tu wauane wao kwa wao.
 
Kinyume chake ndio sahihi, Osama ni muiran au msaudi? waliotekeleza ugaidi wa 9/11 ni 15 kati 19 ni wasaudi, alqaeda, isis wote ni sunni wenye mrengo wa kiwahabi unaofadhiliwa na Saudia, hakuna hata muiran hata mmoja alieshiriki katika ugaidi mkubwa na Iran haijavamia nchi nyingine yoyote kwa kipindi cha miaka 200

Unaijua historia ya Iran wewe??? hebu nenda kaisome tena
 
Iran nitaifa imara na linaamini kitu anachokifanya na hata wananchi wa Iran wanaimani na nchi yao. Marekani atafanya kila analoweza lakin kwa Muiran atachemka tuu
 
Kama tulisema hayohayo vikwazo vyao na washirika wao vimefikia wapi....?
Tangu waanzishe hivyo vikwazo Iran bado haijateleleka na msimamo wao upo palepale....

Iraq na Libya usifananishe na taifa Iran ukae ukijua.
 
Back
Top Bottom