Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki agoma kula kuwaunga mkono wapalestina

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,830
20,257
Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Kanisa Katoliki ameamua kususia kula chakula ili kuonyesha mshikamano na uungaji mkono wake kwa Wapalestina waliosusia kula katika magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Gregory III Laham, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki katika maeneo ya Mashariki Yote, Alexandria na Quds Tukufu mwenye umri wa miaka 83 amejiunga na harakati hizo za kususia kula kuonyesha uungaji mkono wake kwa wafungwa wa Kipalestina.
Shirika la habari la al-Wattan linalopeperusha matangazo yake kwa lugha ya Kiarabu limeripoti kuwa, kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Kanisa Katoliki licha ya umri wake mkubwa amechukua hatua hiyo kukosoa ukandamizaji wanaofanyiwa wafungwa wa Palestina katika magereza ya kutisha ya utawala pandikizi wa israel.
Haya yanajiri siku chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon, Salim Al Hooss kujiunga na mgomo huo wa kula, huku akiulaani vikali utawala haramu wa Israel kwa kukiuka sheria za kimataifa kuhusu mateka na wafungwa wa Kipalestina na kutangaza kuwa, ameanza kususia kula ili kuwaunga mkono mateka hao.
Tangu tarehe 17 ya mwezi uliopita wa Aprili zaidi ya Wapalestina 1,700 wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala haramu wa Israel walianzisha mgomo usio na muda maalum wa kususia kula chakula kulalamikia vitendo vya ukatili na vya kinyama pamoja na hali mbaya ya huduma na mazingira inayowakabili katika jela hizo.
Mgomo huo unaongozwa na Marwan Al-Barghuthi kwa kaulimbiu ya "Uhuru na Heshima" katika magereza yote ya utawala wa Kizayuni.
Source:parstoday
My take; Go padri go hakuna atakayeweza kuuvunja ukiristo kwa kuwa mpinga kristo(israel) Kama mpinga kristo mpya ila watashindwa kwa jina la yesy
 
Atakuwa ameshiba vya kutosha huyo hajui huo mgogoro ulishaondoka na roho za watu ambao walionekana kupinga matakwa ya wazayuni
 
Subiri wayahudi waTZ wakuje, utasanda mjomba.

Sasa ukitaka uwatoe povu waulize ilikuwaje wakamuua Yesu hilo povu watakalotoa
 
Huo mgogoro hautakaa uishe milele.... Ni wa kibiblia zaidi..... Hata huyu padre nadhani amepitiwa kdg.... Asome tuu hiyo biblia ataona kuwa mgogoro huo hauna mwisho
 
Nikiwa kama mkristo naona anachofanya askofu ni sahihi. Ukristo ni Upendo. Hata hivyo wanaoteseka wale ni viumbe vya Mungu na wote wanaowatesa wanafanya dhambi mbele za Mungu aliye hai. Hakuna kutazama hili kiudini. Wala ukristo hausemi mtu amtese mwingine.

Kuna waislamu na wakristo hawajui ukristo.

Kuna waislamu wanaangalia kila jambo kwa muktadha wa dini.
 
Subiri wayahudi waTZ wakuje, utasanda mjomba.

Sasa ukitaka uwatoe povu waulize ilikuwaje wakamuua Yesu hilo povu watakalotoa
Kekereenkede

Ni kama hawa nywele ngumu wa kariakoo na ngozi nyeusi, pua pana ya kibantu eti huwa wanajiita Waarabu, kisa tu wanajua kusema Asalaam Aleykum.
 
Back
Top Bottom