Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,976
Mkuu amedai kuwa anaowateua hawajamwelewa bado! Sijajua kama amejiuliza kuwa kwa nini mpaka sasa hajaeleweka!
Kama bado ngoja nimweleweshe:
1. Kutokutabirika. Mpaka sasa Mkuu hajatabirika. Amedai kuwa anatumbua wa vyeti feki lakini bado wengine, akina Bashite amewaacha kwa very simple reason kuwa ni wachapa kazi!
Pia wengine wanasimamishwa ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma zinazowakabili lakini wengine wanapandishwa vyeo! Hii inawafanya wateuliwa kukosa mwelekeo, wanashindwa kujua ni wakati gani wa kumfurahisha bwana mkubwa na wakati gani wa kumkasirisha! Ukiwaambia wachape kazi tu bila kujua wanachapaje kazi ni shida!
2. Kudhalilishwa hadharani. Wateuliwa baadhi yao wamedhalilishwa hadharani utafikiri watoto wadogo! Hii inawafanya pia wasijiamini na kukata tamaa!
3. Kutokushaurika. Mkulu alidai hadharani kuwa yeye ni mtu anayejiamini na hashauriwi na mtu yeyote na ukimshauri ndio unaharibu kabisa.
Nani sasa atakayepeleka pua kwake kumshauri! Inawezekana Kanuni hazijasainiwa kuna sababu ila nani ataenda kujieleza? Ni ngumu!
Kwa hali hii kutokueleweka kutaendelea tu as long as status quo haitabadilika na asimlaumu mtu yeyote! Haiwezekani mtu uliyemteua wewe tena kwa mkesha leo unamwona hafai! Ni wakati wa kujichunguza mwenyewe!