Zamani ili uweze kuwafikia mashabiki wako lazima utatumia redio na TV na baadhi ya wamiliki walitumia kama fimbo ya kuwachapa wasanii wasio kubaliana nao. Ila siku hizi digital platform na social networking like Insta, fb, Boombplay YouTube nk, vina nguvu kuliko redio na TV na jamaa kaishika haswa na anajua kuitumia. Ndio maana siku hizi hata mbele msanii anaweza akachia album kwa kuposti cover to IG au fb bila ya kufanya media tour na bado album au nyimbo ikafanya vizuri mf Eminem, jay z, Beyonce, j Cole, Childish Gambino mwaka huu wameachia kwa kupitia social media kama njia ya kufanya promo. Kama kipindi kile cha nyuma matumizi ya digital platforms na social networking , zingekuwa na nguvu kama hivi sasa basi naamini, Hip hop ingekuwa bado inasimama na hata hao wasanii wanao baniwa wangekuwa bado wana trend, ila kwa sasa ni ngumu sana kumbania msanii anaye trend ktk social networking na digital platforms.