XXX majuzi
alikuwa nyumbani kwao. Katika pita pita akakutana na Mmakonde mmoja
aliyekuwa anauza vinyago. Alivutiwa sana na kinyago kimoja kilichokuwa
kinafanana na panya. Kilichongwa kwa ustadi kiasi ya kwamba hata manyoya
ungedhani ni yenyewe; wacha kichwa, miguu, mkia na vingine. Akamwuliza
huyo Mmakonde anauzaje hicho kinyago. Akaambiwa ni shillingi mia tano na
kikiiisha nunuliwa hakirudishwi. XXX akaona hiyo ni bei poa kwani ni
kama bei ya soda. Alilipa mara moja akaondoka nacho.
Hajafika mbali, maajabu yakaanza kutokea. Kila aina
ya panya wakaanza kujitokeza majumabani, vichakani, mashimoni na
kwingineko wakimfuata XXX akaingiwa na woga na kuanza kukimbia. Lakini
wapi. Panya waliongezeka na kuongeza kasi yao. Woga ulimzidi huku
akijiuliza afanye nini.
Hapo alipokuwa ni karibu na mto. . Basi akakikimbia
kuelekea huko na panya walikuwa bado wanamfuata na wakiongezeka. Kufika
kwenye kingo za mto huo mkubwa, alikitupa kile kinyago majini na hapo
ndipo maajabu yalipotokea. Wale panya wote waliokuwa wakimfuata,
walikifuata kile kinyago huko majini, wakazama nakufa.
Kuona hayo,XXX ilikuwa ni kama amefunuliwa. Aliondoka
kwa kasi mithiri ya farasi, akielekea kwa yule Mmakonde. Mara kufika
Mmakonde akawa mkali.
Nilichema uchirudishe
Tulia Baba. Una kinyago kinachofanana na Dr. Slaa.
China. Tena nakwambia China kabisa
XXX kesho yake alikata tiketi kwenda China.
HAIJULIKANI XXX ALIRUDI NA NINI KUTOKA CHINA