Kingunge: Mwacheni Magufuli afanye kazi, tumpime baada ya siku 100

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,817
Msimuingilie ingilie muacheni afanye kazi tuliomtuma hayo ni maneno ya Mzee Kingunge swahiba mkubwa Lowasa!

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru, amesema atampima na kuzungumzia utendaji wa Rais wa tano, John Magufuli atakapotimiza siku 100 Ikulu.

Dk. Magufuli leo ametimiza siku 59 tangu kuapishwa kushika madaraka hayo Novemba 5, mwaka jana na ameshafanya mambo makubwa yaliyompa sifa kem kem kitaifa na kimataifa.

Kingunge ambaye mwishoni mwa mwaka jana alikihama chama alichokiasisi cha CCM na kukitumikia kwa zaidi ya miaka 60, jana alisema kwa kawaida watu hupimwa utendaji wao wa kazi zinapofika siku 100.

Kingunge ambaye alikuwa na kadi namba 8 CCM kabla ya kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi kumpigia kampeni aliyekuwa mgombea wa Chadema kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa, alisema ni mapema mno kujadili utendaji wa serikali ya Magufuli.

“Jamani nadhani ni mapema mno, msiwe na haraka nitatoa maoni yangu kuhusu utendaji wake muda huo utakapofika. Kwa sasa mwacheni afanye kazi zake msimwingie ingilie," alisema Kingune ambaye amewahi kushika nyadhifa nzito nzito serikalini.

"Kwani nyinyi mna haraka gani mpaka mnataka nitoe maoni yangu leo?" Aliuliza. "Bado ni mapema sana kumpima.”

Kingunge alisisitiza kuwa ni vyema Magufuli akaachwa afanye kazi zake kwa sasa.

Oktoba 4, mwaka jana, Kingunge alitangaza rasmi kujiengua ndani ya chama hicho, akisema alifanya hivyo kutokana na kile alichoamini kuwa CCM haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa misingi bora na waasisi wake.

Wakati akitangaza uamuzi huo, Kingunge alisema hakusudii kujiunga na chama chochote cha siasa nchini bali atakuwa mtanzania huru, lakini muda si mrefu akaungana na Ukawa kumnadi Lowassa.

Mwanasiasa huyo ambaye sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa CCM, alisema wananchi wanataka mabadiliko na wasipoyaona ndani ya chama hicho watayatafuta nje ya chama, ikiwa ni nukuu ya nasaha maarufu ya Baba wa Taifa, hayati Julius Nyerere aliyowahi kuitoa enzi za uhai wake.
 
Last edited by a moderator:
wengi walioondoka ccm ni kuwa walikuwa wamechoka usanii wa incompetent jk na wala sio ccm as a whole,ndio maana hutowasikia akina kingunge na sumaye wakiukosoa sana utawala huu sababu maigizo ya pombe yana nafuu kidogo.
 
Watu wengi walijua Rais Dr Magufuli angekuwa wale wale. Tunangojea hapawe Uwenyekiti wa chama hatumbuwe majipu kwani JK anacheka nao tu.
 
Mzee Kingunge unataka mambo gani tena ndani ya siku 100 wakati Lowassa ulikuwa unamkubali kuwa atakuwa rais mzuri hata kabla ya kumpeni kuanza, Mzee Kingunge hamna namna tena zaidi ya kumkubali Dr.Magufuli.
 
Kingunge akimsaliti Lowasa atawajua vijana wa Bavicha maana wao huwa hawaogopi wazee ni kuwanywea mbege na viroba na kuwatandika matofali....
 
Kingunge mbona unatuchanganya!! Mtu ambaye alipita kwa kupindisha katiba ataachwaje afanye kazi? Mtu ambaye ameishiwa pumzi atawezaje kufanya kazi na utatumia vigezo gani kumpima? .....

Pamoja na hayo huwa sisahau msemo wako maarufu wa....."Unachukua....Unaweka.....Lowassa"
 
Mungu amlinde atakapotoa kauli yake baada ya siku 100. Akikosea tu, Dawasco wanamletea bili nyingine.
 
Ni maneno ya busara tu toka kwa huyu Mzee. Wanaombeza kwa kuwa aliamua kujiweka kando na siasa za Chama chake cha zamani wanakosea. Ni haki yake kama mtu aliyeona mengi na kuyaasisi mengi katika taifa hili kutoa mawazo na tathmini. Kama alivyoshauri baada ya siku 100 basi atatoa tathmini.
 
Msimuingilie ingilie muacheni afanye kazi tuliomtuma hayo ni maneno ya Mzee Kingunge swahiba mkubwa wa fisadi Lowasa!

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru, amesema atampima na kuzungumzia utendaji wa Rais wa tano, John Magufuli atakapotimiza siku 100 Ikulu.

Dk. Magufuli leo ametimiza siku 59 tangu kuapishwa kushika madaraka hayo Novemba 5, mwaka jana na ameshafanya mambo makubwa yaliyompa sifa kem kem kitaifa na kimataifa.

Kingunge ambaye mwishoni mwa mwaka jana alikihama chama alichokiasisi cha CCM na kukitumikia kwa zaidi ya miaka 60, jana alisema kwa kawaida watu hupimwa utendaji wao wa kazi zinapofika siku 100.

Kingunge ambaye alikuwa na kadi namba 8 CCM kabla ya kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi kumpigia kampeni aliyekuwa mgombea wa Chadema kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa, alisema ni mapema mno kujadili utendaji wa serikali ya Magufuli.

“Jamani nadhani ni mapema mno, msiwe na haraka nitatoa maoni yangu kuhusu utendaji wake muda huo utakapofika. Kwa sasa mwacheni afanye kazi zake msimwingie ingilie," alisema Kingune ambaye amewahi kushika nyadhifa nzito nzito serikalini.

"Kwani nyinyi mna haraka gani mpaka mnataka nitoe maoni yangu leo?" Aliuliza. "Bado ni mapema sana kumpima.”

Kingunge alisisitiza kuwa ni vyema Magufuli akaachwa afanye kazi zake kwa sasa.

Oktoba 4, mwaka jana, Kingunge alitangaza rasmi kujiengua ndani ya chama hicho, akisema alifanya hivyo kutokana na kile alichoamini kuwa CCM haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa misingi bora na waasisi wake.

Wakati akitangaza uamuzi huo, Kingunge alisema hakusudii kujiunga na chama chochote cha siasa nchini bali atakuwa mtanzania huru, lakini muda si mrefu akaungana na Ukawa kumnadi Lowassa.

Mwanasiasa huyo ambaye sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa CCM, alisema wananchi wanataka mabadiliko na wasipoyaona ndani ya chama hicho watayatafuta nje ya chama, ikiwa ni nukuu ya nasaha maarufu ya Baba wa Taifa, hayati Julius Nyerere aliyowahi kuitoa enzi za uhai wake.

hana lolote MNAFIKI mkubwa huyo kwani ANAJIBALAGUZA kwakuwa anajua muda wowote kuanzia sasa kuna KESI ya aibu dhidi yake itafunguliwa baada ya DAWASCO kugundua alichokuwa akiwafanyia wakazi wa kuanzia tegeta, wazo hadi bunju kwa kutumia yale MABOZA yake. naomba niishie tu hapa kwa leo na niwapishe wengine waendelee.
 
KAZI NI TUNU YA MAISHA ATA KABLA UJAZALIWA NA NDO ZAWADI MUNGU ALIYOTUPATIA... SO NASUBIRI MATUNDA YA KAZI ANAYOFANYA RAISI WETU
 
Kingunge akimsaliti Lowasa atawajua vijana wa Bavicha maana wao huwa hawaogopi wazee ni kuwanywea mbege na viroba na kuwatandika matofali....

Ha ha ha ahaaaaa ha haaaaaaaaaaaaaaa hata sijui umewaza nini kuandika hivi. Nimecheka sana mpaka walio pembeni yangu wamebaki kunishangaa. Asante kwa kunitanua mbavu zangu. JF idumu milele.
 
Mzee Kingunge unataka mambo gani tena ndani ya siku 100 wakati Lowassa ulikuwa unamkubali kuwa atakuwa rais mzuri hata kabla ya kumpeni kuanza, Mzee Kingunge hamna namna tena zaidi ya kumkubali Dr.Magufuli.
Kama wewe ulivyokuwa unamuunga mkono Membe na sasa unamshabikia Magufuli baada ya Membe kubwagwa.
 
Back
Top Bottom