King James Version (1566–1625)

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
13,569
Reaction score
40,788
King James I (1566–1625) ndiye aliyeagiza tafsiri ya Biblia maarufu ya “King James Version,” lakini hakuandika Biblia hiyo mwenyewe. King James hakuwa kiongozi wa kidini alikuwa mfalme wa Uingereza na Uskochi (1566–1625). Alitoa agizo la kutafsiri Biblia (iliyokuja kuitwa King James Version – KJV) kwa

Sababu kuu la Agizo lake la tafsiri ya biblia zifuatazo:

1. Kuondoa migawanyiko ya kidini:
Wakati huo kulikuwa na migogoro kati ya Waprotestanti, Wakatoliki, na Puritani Alitaka tafsiri moja ya Biblia ambayo ingeruhusu umoja wa taifa chini ya mfalme.

2. Kudhibiti ushawishi wa tafsiri zilizopo: Tafsiri zilizokuwepo, kama Geneva Bible, zilikuwa na maelezo ya pembezoni yaliyomkosoa mfalme. Alitaka tafsiri isiyo na maelezo ya kupinga mamlaka ya kifalme.

3. Kuimarisha mamlaka yake kisiasa: Kwa kuwa mfalme aliaminika kuwa kichwa cha Kanisa la Uingereza (Anglican Church), aliona tafsiri rasmi kama njia ya kuhalalisha uongozi wake wa kiroho na kisiasa.

Madhaifu ya tafsiri ya Biblia ya King James.

1. Imetafsiriwa kwa lugha ya zamani (Old English) Maneno kama “thou, thee, ye, hath, shalt” ni magumu kwa wasomaji wa sasa kuelewa.

2. Ilitafsiriwa kabla ya ugunduzi wa maandiko ya kale zaidi KJV ilitafsiriwa mwaka 1611, kabla ya kupatikana kwa Dead Sea Scrolls (karne ya 20) na maandiko mengine ya zamani yaliyo sahihi zaidi.

3. Imetegemea maandiko ya Kigiriki ya baadaye (Textus Receptus) ilitumia maandiko ya Kigiriki yaliyo na makosa ya nakala tofauti na tafsiri mpya zinazotegemea Alexandrian manuscripts ambazo ni sahihi zaidi.

4. Inaongezea maneno ambayo si ya asili KJV huongeza maneno kwa ufafanuzi bila kuyatofautisha, hivyo msomaji hawezi kutofautisha yaliyo ya maandiko ya awali na ya kuongezewa.

5. Baadhi ya aya si sahihi au hazipo katika maandiko ya kale
Mfano: Yohana 5:7-8 inaongezea dhana ya Utatu (Trinity) ambayo haipo kwenye maandiko ya kale zaidi.

Aya nyingine kama Marko 16:9–20 na Yohana 7:53–8:11 zina utata kuhusu uhalali wake.
 
Wewe Kuingia Peponi Kwako- Utahukumiwa na Mungu kuendana na Bibilia ya aina yeyote ile iwe ya king James,Jerusalem Bible etc. So tuliza Mihemko endelea na Dini Yako .unapoteza Muda na kughafilisha akili zako badala ya kufanya yakupasayo ili uweze enda Kwenye Pepo ulioandaliwa na Mola wako.ambayo ni tofauti 100% na ya Hawa wenye Bibilia Yao na Wala upati chochote cha maana kupoteza muda wako kuongelea Ukristo
 

Attachments

  • ssstwitter.com_1753774036611.mp4
    4.6 MB
Nigawie kidogo mahela Mkuu kwa kuwa mvaa kobazi Mwandamizi JF wa kukandia Wakristo ukilipwa ujira ila sisi Wapagani, Wahindu, Wabudha, Wayahudi, Rastafarians tunakula bata na hatuhangaiki kamwe na dini zisizotuhusu 🙎

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Mkuu mbona unajaziba unapingana na maandishi ya historia na biblia yenyewe mimi sijatia neno langu hapo.
 
Mkuu katika huo uzi nimekandamizia wapi wa ukristo haya ni maarifa nilio soma leo asaubuhi hapa maktaba ya kanisa kama ni mabaya mbona yapo hapa yamehidhiwa.
 
Ni kawaida yao wakikosa hoja au majibu kukimbilia upande mgine au mods kuhamisha uzi ili wanusurike na aibu ya kurishwa matango pori
 
Mkuu mbona unajaziba unapingana na maandishi ya historia na biblia yenyewe mimi sijatia neno langu hapo.
Sina Jazba mkuu nipo nnatoa mapepo karibu unisaidie.
 

Attachments

  • ssstwitter.com_1752599098510.mp4
    3.4 MB
Sina Jazba mkuu nipo nnatoa mapepo karibu unisaidie.
Acha hizo we ni mtu mzima acha kujitowa fahamu kama chizi, fanya correction au pinga kwa hoja mkuu.
 
Acha hizo we ni mtu mzima acha kujitowa fahamu kama chizi, fanya correction au pinga kwa hoja mkuu.
Nambie wewe hasa unataka kujua Nini katika Ukristo ,Bibilia na juu ya ulimwengu ili nikupe majibu stahiki- ila tu Usije sema nakashfu Imani yako.Karibu
 
Ni kawaida yao wakikosa hoja au majibu kukimbilia upande mgine au mods kuhamisha uzi ili wanusurike na aibu ya kurishwa matango pori
Hivi Ushaidi wako wewe kuwa Bibilia ina makosa Unao?? Weka hapa tuone! Aiingii akilini unaposema Bibilia imechakachuliwa wakati uweki ushaidi wowote..hii ni sawa kumpeleka mtu mahakamani ukilala Mika amekuibia pasibo ushaidi wa macho🤣Matango pori yako wapi katika Bibilia honyesha basi tukuamini tufutae vile unavyotaka.Kingine Wakristo Toka Karne ya 7 walishamaliza kujua Imani zote na dini zote zilizopo Duniani na Kuna Vitabu vyake juu ya hayo so usifikirie wewe ndo mjuzi wa haya mambo wewe ujui chochote cha maana kuhusu Ukristo,Bibilia na ata hiyo Imani uliyonayo
 
Baadhi ya aya si sahihi au hazipo katika maandiko ya kale
Mfano: Yohana 5:7-8 inaongezea dhana ya Utatu (Trinity) ambayo haipo kwenye maandiko ya kale zaidi.

Bro Covax. Habar za mchana.

Umepotosha kwenye maandiko.
Hakuna utatu kwenye hilo andiko.

Yohana 5 : 7 -8
"Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. 8 Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. 9 Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda."

Aya nyingine kama Marko 16:9–20 na Yohana 7:53–8:11 zina utata kuhusu uhalali wake.

Hakuna Yohana 7 : 53
Imeishia mstar wa 52.

Pia sijui kama umezisoma. Na kama umezisoma hebu tuambie Uhalali wa nini ay nani unaongelea hapo?.

Ili nikusaidie kujibu
 

Huyu jamaa ana shida ya uelewa wa Biblia.

Anautaka sana Ukristo sema ndio uelewa wake mdogo.

Ila taratibu atakaa sawa.
Ntakuwa namjibu hoja zake.
 
Mkuu katika huo uzi nimekandamizia wapi wa ukristo haya ni maarifa nilio soma leo asaubuhi hapa maktaba ya kanisa kama ni mabaya mbona yapo hapa yamehidhafiwa.
Umepotosha Umma.

Maandiko yasiyo ya Ukweli yanaweza kuleta taharuki.

Hebu kama uko hapo Maktaba rudia kusoma hivyo vifungu.

Otherwise Hoja na Uzi wako wote Umedanganya Wana JF.
 
Shetani ndiye mwandishi wa thread hii, ameandika akiwa amemkalia Covax kama kiti.
 
Ni kawaida yao wakikosa hoja au majibu kukimbilia upande mgine au mods kuhamisha uzi ili wanusurike na aibu ya kurishwa matango pori
Nimekujibu bro.

Mm nishakuambia siwez kimbia hoja zako.

Na ww pia kuwa Muungwana.

Rekebisha yale maandiko au
Omba msamaha kwa JF kwa kuleta maandishi yasiyo sahihi.
 
Huyu jamaa ana shida ya uelewa wa Biblia.

Anautaka sana Ukristo sema ndio uelewa wake mdogo.

Ila taratibu atakaa sawa.
Ntakuwa namjibu hoja zake.
Aje tumpe Neno Amkiri Yesu Kristo alie Bwana na Mokozi,aijue KWELI nayo KWELI itamweka Uhuru !! Kwanza ajiulizi kwa Nini Mapdre wa Kikatoliki awapayukipayuki mitaani wakiubiri au kusema lolote juu ya Uislam au Budha,Au Kulazimisha Watu waingie katika Imani Katoliki?? Anafikiri kuwa na elimu zao zote walizo nazo ni Wapumbavu??Padre wa Kikatoliki anatakiwa kuwa na 2 Degrees ndo apewe Upadre-Jesuit 4 Degree ...utawafananisha na Walimu wa Madrassa au imamu??

Rum 14:11
Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.
KUKU WAKO UMKIMBIZI MCHANA KWANI JIONI ATARUDI TU NYUMBANI KWENYE BANDA LAKE KIULAIINI UTAMSHIKA.ipo Siku utakutana na MUNGU wa KWELI macho kwa Macho wewe na Yeye tu .Wawili :hapo ndo itajulikana Mbivu na mbichi
 

Unajua Jamaa ana google sana alaf analeta kwa Jamii bila kufanya uhakiki.

Mm nina app ya Biblia kwa simu na pia kwenye chrome yangu kuna bookmarks ya quran.

Kwenye Hoja zenye andiko liwe la Biblia au quran linalowekwa JF huwa naenda kuangalia kama maandishi ni sahihi.

Na sio mtu kuokota tu huko facebook na kuweka kwa Jamii.
 
Alafu ajui kuwa anapigana Vitu visio na faida yeyote kwake na pia anazidi kujichanganya akili yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…