Kinana nenda Ikulu bana!

Kinana nenda Ikulu bana!

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Nakerwa na tabia ya Mh Kinana ya kuzuunguka nchi nzima na kuiponda serikali yake ya CCM mbele ya wananchi kuwa haishughulikii matatizo ya wananchi, hivi hii ni sawa au CCM inatapatapa? Kwanini Kinana asifanye mikutano ya ndani na viongozi wa serikali yake ya CCM kuhusu kero za wananchi anazokumbana nazo wakati anapofanya ziara zake mikoani badala ya kutumia vyombo vya habari kuilaumu serikali yake. Hii ina maana gani?, hii ina malengo gani? hapa anakusudia nini? anataka wananchi wamueleweje?. Hivi viongozi wakuu wa chama kama Kinana wanazuiwa na nani kukutana na kuongea na viongozi wakuu wa serikali kuhusu utendaji mbovu au mzuri wa serikali ya CCM kwa wananchi? Kila mtu anakerwa na tabia ya Kinana kuivua nguo serikali yetu mbele ya wananchi. Hii inasababisha wananchi pia waichukie na kuidharau serikali yao pia kama Kinana anavyoiponda serikali yake mbele yao. Kama kinana anakiri kuwa serikali ya CCM ni mbovu je sisi wananchi? Maana kama mtoto wa mbwa ni mbwa pia, na serikali yetu ni mtoto wa CCM, sasa sisi tusemeje hapo? Ataweza vipi kuitenganisha tabia ya serikali na tabia ya chama chake cha CCM? Hii ni mbinu potovu itakayotuharibia chama.
 
kinana waajabu sana alikuja hapa nyamongo tukamweleza habari ya mkuu wa wilaya alivyo timua mwenyekiti wa kijiji cha nyakunguru kwa tiketi ya ccm akaweka wachadema kinana wakiwa nape wakaonyesha kushangaa na na kumtaka dc ajieleze na kukiri wakatupa moyo kwamba watahakikisha dc huyo anahamishwa kwa kusaliti chama chetu hadi leo hamna chochote kilichofanyika kinana na nape ni kaboboo tu hakuna lolote
 
ufalme ukujifitini wenyewe ni dalili ya kuanguka!
 
Back
Top Bottom