Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
Hakika ''muda hutupa majibu'' na ''uzoefu ni mwalimu mzuri''. Ukifuatilia kwa kina chanzo cha siasa za upinzani hasa CHADEMA kukosa 'consistency' hii imechngiwa kwa kiasi kikubwa na 'uchanga' wa wafuasi wake ambao wengi wanakuwa wa hujiunga pale wanapomaliza shule au vyuo kwa 'msukumo rika' na kisha baada ya muda hujikuta wameachana na siasa hasa pale wanapoanza maisha ya majukumu ya kifamilia.
Nimejaribu kufuatilia, kutokana na 'uchanga' wengi hawana uvumilivu dhidi ya hoja kinzani na huishia kutukana na kejeli na chuki isiyokuwa na chanzo, yaani unamchukia mtu sababu ana mawazo tofauti na wewe, utasikia ''hujielewi'' nk. Kawaida ya chuki ikizidi hufikia mahala hali ya kukata tamaa huja na hapo ndipo hasa wengi wa vijana hawa hujikuta wameachana na siasa za upinzani na kuwa 'neutral' au kujiunga na CCM. Ni sawa na vijana wa kidato cha pili 'hawaambiliki', wakorofi na wajuaji lakini wakishavuka hujuta na kubadilika.
Sababu kubwa ya kuwa wenye jazba hutokana na ghiliba za viongozi wanaowashawishi kujiunga na chama chao. Mara nyingi huwashawishi kwa kuwatia hasira ''tunaibiwa, mimi nikiingia madarakani nitagawa pesa bila kufanya kazi' nk nk nk..pia siasa za kudanganywa 'huyu ndiye mwizi mkuu, ndiye adui namba moja wa maisha yetu'' kisha baada ya muda viongozi hao hao huishia kumkaribisha na kukanusha waliyoyasema. Kwa muda mfupi hii imevutia wanachama ila kwa muda mrefu binadamu hujiuliza na kugundua ulaghai uliopo na kisha kukata tamaa.
Kwa sasa hata ukifuatilia mitandaoni utagundua wafuasi wakubwa wa upinzani hawajui historia za viongozi wao au washika bendera wao. Hawajui ya kwamba vyama vyao vilipata hadhi baada ya kuwadhalilisha hao ambao sasa wanaitwa 'wafalme' na kupewa kushika bendera za vyama vyao. Ndio maana siku za karibuni kambi nzima ya upinzani imegeuka na kumsifu Raisi mstaafu Jakaya Kikwete angali waliongoza kumkashifu hadi kufikia kuitisha maandamano JK asizidishe hata siku moja Ikulu, Nasema huu ni 'uchanga' na ukosefu wa historia na ndio sababu kuu leo badala ya kujenga na kujibu hoja upizani wa Tanzania umeishia kutukana na kutoa kejeli.
Muwe na Jumamosi njema.