Profesa
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 905
- 624
Kinachoendelea naweza kukifananisha mechi ya Simba na Yanga au Mabingwa wawili wa NGumi.
Huku wananchi wakipambana kuweka dau nani zaidi, na wengine wakikaa kimya kama washabiki wa Arsenal wakisubiri siku ya kushinda ndio washangilie lakini siku nyingine wanawaachia washabiki wa Man U, kinachoendelea hakina maslahi yeyote kwa nchi hii kwa sasa, zaidi ya kuinufaisha media kuendelea kufanya biashara, na hawa viongozi wawili kunufaika kiumaarufu wa nani mwenye vijembe au mbinu zaidi ya mwingine.
Pale nchi inaposimama na kuanza kujadili maslahi binafsi ya watu wawili ambao wanashindana kuchafuana, kwa mamlaka na ushawishi walionao, ni hatari sana. Maana watu hawa wanapoteza logic na kamwe hawataweza kusimamia majukumu yao yanayowapasa.
Wakati umefika sasa wanachi kuacha kushabikia huu upuuzi na kuukemea. Askofu atueleze habari za Yesu sio za Makonda, na Makonda autueleze mipango ya maendeleo Mkoa wa Dar es Salaam, na atuambie serikali imekusudia nini na sisi tutashiriki vipi sio habari za Gwajima au kuchokonoa ili kuonyesha ana uwezo wa kumshinda. Wote hawa bado wana nafasi kubwa kabisa ya kushinda au kuwa maarufu kwa kusimamia vyema maeneo yao ambayo wana mamlaka nayo.
Naamini Askofu sio mwanasiasa, na Makonda sio mwanasiasa, sasa mbinu zao za utawala ni kama za kisiasa. Zinakera, haziwasaidii waumini wala wananchi wa Dar es Salaam.
Naomba wahusika wawasihi hawa wawili waachane na huu mchezo waendelee na majukumu yao binafsi yanayowakabili. Tumechoka kusikia huu upuuzi.
Kama ni swala la madawa ya kulevya Makonda kashadhibitiwa na mamlaka husika na chombo kinachohusika kikishawishika watuhumiwa bado wana makosa basi kitaendelea na taratatibu.
Kama kuna anaona kaonewa, aende Mahakamani kudai haki, aache kuupotosha uma kwa kutuletea mashindano ya kuchafuana ambayo kimaadili hayajengi, tunawafundisha nini watoto wetu na vijana kuhusu namna bora ya kushughulikia maslahi ya nchi? Tunaomba Mamlaka husioka ziingilie kati zikemee tabia hii chafu isiyo na maslahi kwa nchi!
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.