Kwetunikwetu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 1,535
- 418
Mzee wetu Mhe. FREDERICK SUMAYE atueleze nini kinaendelea kati yake na viongozi wakuu wa CHADEMA? Ni juzi tu tarehe 16 Juni majira ya sa 3.15 asubuhi maeneo ya Protea Hoteli iliyopo Oysterbay nilimuona kwa MACHO YANGU mheshimiwa huyu akiwa kwenye gari yake aina ya Landcruiser namba T634 AKN akipokelewa na vigogo wa CHADEMA akiwemo Mhe. MBOWE, DR. SLAA na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA BOB MAKANI na kuelekea kwenye chumba cha mikutano. Walijifungia kwenye chumba hicho takribani saa mbili na zaidi hadi mishale ya saa 5.20 hivi asubuhi ndipo kigogo huyu alipoondoka eneo hilo. Uswahiba huu umeanza lini??
Nampa HEKO! Napenda kumweleza kuwa kama CHADEMA wamempenda basi atueleze tumpigie debe kwani hadi sasa CHADEMA haijawa wazi nani atagombea kinyangányiro cha kiti cha Urais mwaka huu wa uchaguzi. Pengine bado CHADEMA wanawinda majeruhi wa CCM??
Rai yangu kwa Mheshimiwa SUMAYE ni kwamba, haki kikatiba anayo inayomlinda katika upigaji na upigiwaji wa kura ila mzee, wenzio wa upande wa pili wanayo taarifa hiyo? Au unacheza rafu?
Namtakia kila lililo kheri kwenye mazungumzo yake kuelekea utekelezaji wa demokrasia.
Kuwa wazi, usijifiche una kila haki.
mimi, Chilomo Chiwale
Chilomo Chiwale, hii sasa unaharibu, hata kama ni kweli uliyashuhudia hayo, hizo ni faragha za watu, umezileta hapa ili ama kumuharibia, ama kiharibia Chadema, kwani hata kama alikuwa analitafakari ombi lolote toka Chadema, na kabla hajafikia maamuzi, wakasikia limeibukia JF, si ata ghairi?.
Ndio maana kuna wakati mwingine, unasikia jambo, unashuhudia jambo, unalihifadhi mpaka upate uhakika.
Chilomo unawezekana wewe ukawa ni membe wa kundi la manyoka wa TISS, umetumwa kazini kwako kufuatilia, sasa unamfitinisha na Chadema ili kumuharibia mafao yake?!.
Sumaye ni mtu huru kama walivyo wengine ana uhuru wa kukutana na yoyote popote bila kuvunja sheria yoyote, hivi unajua hata Zitto ni rafiki na JK, ukiwaona wanacheka na kutembeleana, sio ndio utalianzisha Zitto huyooo...CCM.
CHADEMA ENDELEZENI MIKAKATI, SYSTEN ON OPARATION MPAKA NDANI YA JF!
thank you mganyizi kwa kunipa moyo kwani nilishaanza kuogopa kuwa huenda nimekurupuka pia sina haki ya ku share yale niliyoyaona.
Naamini jf ipo kwa ajili ya kujuzana. Najifunza pia. Nimeshakaribia.
Mzee wetu Mhe. FREDERICK SUMAYE atueleze nini kinaendelea kati yake na viongozi wakuu wa CHADEMA? Ni juzi tu tarehe 16 Juni majira ya sa 3.15 asubuhi maeneo ya Protea Hoteli iliyopo Oysterbay nilimuona kwa MACHO YANGU mheshimiwa huyu akiwa kwenye gari yake aina ya Landcruiser namba T634 AKN akipokelewa na vigogo wa CHADEMA akiwemo Mhe. MBOWE, DR. SLAA na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA BOB MAKANI na kuelekea kwenye chumba cha mikutano. Walijifungia kwenye chumba hicho takribani saa mbili na zaidi hadi mishale ya saa 5.20 hivi asubuhi ndipo kigogo huyu alipoondoka eneo hilo. Uswahiba huu umeanza lini??
Nampa HEKO! Napenda kumweleza kuwa kama CHADEMA wamempenda basi atueleze tumpigie debe kwani hadi sasa CHADEMA haijawa wazi nani atagombea kinyangányiro cha kiti cha Urais mwaka huu wa uchaguzi. Pengine bado CHADEMA wanawinda majeruhi wa CCM??
Rai yangu kwa Mheshimiwa SUMAYE ni kwamba, haki kikatiba anayo inayomlinda katika upigaji na upigiwaji wa kura ila mzee, wenzio wa upande wa pili wanayo taarifa hiyo? Au unacheza rafu?
Namtakia kila lililo kheri kwenye mazungumzo yake kuelekea utekelezaji wa demokrasia.
Kuwa wazi, usijifiche una kila haki.
mimi, Chilomo Chiwale
Dr Slaa ameshavuka kwa mbali hii ngazi ya UBUNGE. Anaogopa nini kugombea URAIS? Atachelewachelewa kama alivyofanya SAS tangu mwaka 1985 hadi akaja kuchukua fomu 2005! Ikawa tayari kila kitu hakiko upande wake.
Dr Slaa, bila kuikamata IKULU sasa huko mbeleni itakuwa vigumu sana kwako. Wala jitihada zako BUNGENI na ndani ya majukwaa ya CHADEMA havitatusaidia sana WATANZANIA.