Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,504
- 8,253
Wakuu ccm inakata roho kwa tabu sana labda sijui kwa sababu ya madhambi iliyotenda?! Katika jimbo la mwibara kangi aliwanunua washindi wa pili, tatu,nk ktk kura za maoni za udiwani chadema pamoja na viongozi wa chadema wa eneo hilo ili wagombea hao walioshindwa wakachukue form ya kugombea udiwani, cha ajabu mkurugenzi kawapa form lakin kilichotokea ni shida! Makanda wamekinukisha hadi ikabidi wagombea halisi ndo wapewe form na wale mamluki kutenguliwa. Kipindi wanachonga huo mchongo wao kama kawaida makamanda walikuwa wanawachora tu na hako kamchezo kao wakarekodi hadi clip za video ambazo zilitumwa makao makuu ya chama nacho chama kimeshachua hatua kimewaengua karibia viongozi wa eneo hilo.
Kasheshe lingine lilikuwa pale bunda, katika hali ya kushangaza na kutia aibu makada wa ccm walienda kwa mkurugenzi kuzuia esther bulaya asipewe form ya kugombea ubunge, madai yao eti kwa nini apewe aliyeshika nafasi ya tatu aachwe wa kwanza?! Aisee palichimbika kwelikweli pamoja na kwamba aliyeshika namba 1 alikuwepo pale na alisisitiza wao chadema ndo wameamua hivyo sasa wao ccm kinawauma nini?! Lakin maccm yaliendelea kukomaa hadi ikabidu waitwe wanasheria kuja kufafanua hayo mambo kisheria ndipo maccm yakanywea na Esther akachukua form.