kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,785
- 20,164
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameuonya vikali utawala wa kifalme wa Aal-Saud dhidi ya kufanya maamuzi yoyote ya kipuuzi dhidi ya taifa hili na kusisitiza kwamba Jeshi la Iran halitachelewa kutoa jibu kali kwa kuusambaratisha utawala wote wa Riyadh.
Brigedia Jenerali Hussein Dehqan ameyasema hayo katika mahojiano yalioyorushwa jana Jumapili na kanali ya televisheni ya al-Manar inayorusha matangazo yake kwa lugha ya Kiarabu.
Matamshi ya Dehqan ni radiamali kwa kauli ya uhasama iliyotolewa hivi karibuni na Naibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme na Waziri wa Ulinzi wa utawala wa kifalme wa Saudia, Mohammad Bin Salman Al Saud dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Bin Salman hivi karibuni mbali na kudhihirisha chuki yake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kusema wazi kwamba, Saudia katu haitakuwa na mahusiano mazuri na Tehran, alidai kwamba vita vyovyote kati ya Riyadh na Tehran vitafanyika ndani ya ardhi ya Iran na Saudia haitaruhusu vita hivyo vifanyike katika ardhi yake.
Brigedia Jenerali Hussein Dehqan, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefafanua kuwa, Iran itatoa jibu kali kwa chokochoko zozote zitakazoanzishwa na Saudia dhidi yake kwa kuusambaratisha utawala huo wote wa kifalme ghairi ya miji mitakatifu ya Makka na Madina.
Akiashiria namna jeshi la Saudia lilivyoua raia 12,000 wa Yemen mbali na kuharibu miundombinu ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu katika hujuma zake za anga, Dehqan amesema Riyadh isidhani itafanya kile inachotaka kwa kuwa ina jeshi la anga.
Jumatano iliyopita, Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema kauli hiyo ya uhasama ya Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia ni dhihirisho tosha kuwa Riyadh inaunga mkono ugaidi na utawala huo wa kifalme umejengeka katika misingi ya sera haribifu.
Source: ParsToday