Kimbia by Babuu (Langa Verse)

Yu kwapi She mponda,yukwapi Jenerali Komba ,nchi kali ,siri kali ,cheza mbali na Wajomba[emoji95]
 
Mabuti ya kijeshi uyaone mafupi mepesi/
Yani kama vile simple toka nduki toka lesi/
Ka risasi ya bunduki au jeti/
No kunyuti no kuketi, wape nafasi wakushoot/
Kama Malcolm X usikubali kubaki/
Uwe pimbi upewe kesi/
Ikibidi jitose ndani ya dimbwi la kinyesi/
Sio suala la uoga,kuogopa ukunguru/
Ila Bora kurogwa kuliko kukosa uhuru/
Wapi Shemponda wapi Jenerali Komba/
Siri Kali Sera Kali cheza mbali na wajomba/
Kimbiaa, mitihani imevuja nyie hamjasikia!?/
Yanini kusoma huku elimu inanunuliwa/
Kimbiaa, Nchi imeshauzwa hii hamna kusikilizia/
TANESCO, Madini Hadi Air Tanzania/
Watoto wa uswazi hawana matumaini/
Ndoto zao ujambazi sababu ya umaskini/
Matapeli wenye shahada kila hatua tatu/
Makahaba wa miaka kumi na tatu/
Maskani kamsitu, vicheche na machatu/
Usipite pekupeku bila kuvaa viatu/
Aaaah Kimbiaaaaaaaa

Rest Easy LANGA (RIP)
 
Bila video. Waliozaliwa miaka ya karibuni kuelewa hii nyimbo.
Nyimbo hii inataka usikie lile beat na unaicheki ile video.
 
Kiroboto ingekuwa ni mbele angekuwa na hadhi sana. Angekuwa ni bonge moja la icon sema ndo hivyo bongo nyoso.
Nature amefanya kila aina ya style ya Bongo Fleva na nyimbo zilikuwa kali.
True that bongo kuna watu wanaudai mziki sana yani na sioni wao kupata chao...
kiroboto ngoma zake mpaka leo naskiliza na sijui alikua anatumia nn kuandika lyricd zake huyu jamaa

Kuna ngoma flani anaingianna maneno sijui hata aliyapata wapi yani... "tindi ndili ngetitinginye " hiyo ngoma yuko na kina kr mulla
 
Hii beat ya huu wimbo ni ya kibabe sana...

Binafsi naikubali verse ya langa sana

"Mabuti ya kijeshi uyaone mafupi mepesi yani toka nduki toka lesi"
My Timbs start feeling like they Nike Airs on me

Verse ya Jadakiss kwenye wimbo wa "Run" wa Ghostface Killa. Sounds familiar...?
 
My Timbs start feeling like they Nike Airs on me

Verse ya Jadakiss kwenye wimbo wa "Run" wa Ghostface Killa. Sounds familiar...?
Familiar enough... most of our rappers wanatwist tu kidogo mfani Fid Q ngima zake nyingi punch anasample ila ikisikilizika kiswahili inabang zaidi
 
Wakuu naombeni nyimbo hizi mbili
KIMBIA BABUU WA KITAA FT LANGA
KESHO NANUNUA BUNDUKI HAMIDU 26 ft Byser & Young Dsm
 
Marashi ya isymeyak/ukinicheki msafi, sitoki masaki natokea king'oko
Langa atabaki kua best lyrical artist ever kwenye hip-hop ya bongo....
Ukitaka kumficha mwafrika weka ujumbe kwenye kitabu
Mi natumia muziki kufikisha ujumbe Kwa watu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…