"Kill The Boer" Ilivyotikisa The White House

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
289
Reaction score
489
"Dhubul iBhulu! Kill the Boer, Kill the Farmer, Victory is certain".
Kauli tata iliyomuweka kikaangoni Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mbele ya Rais wa Marekani Donald Trump walipokutana mei 21, 2025 Ikulu ya Washington DC.

Je kauli inayomkaanga Ramaphosa ilitoka kwenye kinywa cha nani na ina maana gani inayoleta utata?
Wahenga wanasema "maneno huumba" basi huenda ndio chanzo cha utata wa kauli hii "Dhubul ibhulu" kutoka kwenye lugha adhimu ya kiXhosa likimaanisha " Ua makaburu, yaani "Kill the Boer" kwa kiingereza.

"Dubhul Ibulu" kauli chafu la kihalifu na kibaguzi mbele ya watu weupe wa Afrika Kusini maarufu kama "Afrikeneers" lakini ni neno la kizalendo kwa watu weusi wa Afrika Kusini likitoka kwenye mdomo wa mwanaharakati na mwanasiasa mashuhuri wa upinzani mwenye roho ya chui, Julius Malema.

Kauli hii ni hisia za kidonda kinachotiwa chumvi mbele ya makaburu kutokana na kutumika katika harakati za ukombozi dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini mnamo miaka ya 1980.

"Dubul Ibulu" ndio kauli mbiu iliyomfanya Trump kutoa kibali kuwahamisha raia weupe wa Afrika Kusini "The Afrikeneers" akidai kuwa serikali ya Ramaphosa imeshindwa kuwalinda wakulima hao kwa kuwanyang'anya mashamba na kuwaua akitafsiri kama mauaji ya halaiki "Genocide"

Kwenye video iliyoonyeshwa mbele ya Marais Ramaphosa na Trump anaonekana Malema ambaye ni kiongozi wa chama cha EFF Julius Malema akiimba "Kill the Boer" inampa wakati mgumu Ramaphosa kujitetea akidai kuwa ilikuwa kauli ya kisiasa na haikuwa na madhara na hakuna mauaji yaliyotokea nchini kwake .

Lakini je ni nani huyu, Julius Malema anaye itikisa Ikulu ya Marekani mpaka kuhofia uwepo wake jukwaani?

Julius Malema alizaliwa Machi 3, 1981 huko Seshego katika Jimbo la Transvaal, ni Baba wa watoto watatu akifahamika pia kwa jina la utani "JUJU".

Mwaka 2008 alijiunga na chuo kikuu cha Afrika Kusini UNISA, ambapo alihitimu stashada ya maendeleo ya vijana, Kisha mwaka 2016 alihitimu shahada katika sanaa ya Mawasiliano na Lugha za Afrika.

Ukurasa wake katika shajara ya siasa ulifunguliwa mnamo mwaka 2008 baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa umoja wa vijana wa chama cha ANC.
Alijizolea umaarufu usiopimika akiwa bega kwa bega na Rais wa chama hicho Jacob Zuma ambaye aliwahi kuwa Rais wa Afrika Kusini.
Kama vikombe vinavyoweza kusigana kwenye kabati, basi hata binadamu hushindwana, ilipofika mwaka 2012 uhusiano baina ya Malema na Zuma ulipungua wakawa hawaivi tena kwenye chungu kimoja cha siasa.

Malema alimtuhumu Zuma kujihusisha na kashfa mbalimbali ikiwemo rushwa na ufisadi akiwa Rais wa nchi hivyo alianzisha kampeni ya kumtoa madarakani.
Ilipofika mwezi April mwaka huohuo, Mwezi mmoja kabla ya kikao cha mkutano mkuu wa ANC, Malema alifutwa uanachama wa chama hicho kwa tuhuma za kuchochea migogoro ndani ya chama.

Kujikwaa sio kuanguka, ilipofika mwaka 2013 Malema alianzisha chama kingine chenye mrengo wa kijamaa kikiitwa Economic Freedom Fighters yaani Chama cha kupigania uhuru wa kiuchumi.

Mchicha ukaanza kuonyesha dalili za kuwa kama mbuyu, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2014 EFF kilishinda viti 25 vya ubunge akiwemo Malema mwenyewe, kikiwa chama cha tatu chenye nguvu nyuma ya ANC na DA.
Njia ya mwanaharakati wa upinzani Afrika haujawahi kuwa nyepesi, inajaa miiba, milima na mabonde. Malema amepitia misukosuko mingi ya kisheria, mwaka 2010 alishitakiwa kwa kumhusisha Rais Zuma kwenye tuhuma za ubakaji, na mwaka uliofuata alishitakiwa kwa kauli yake ya uchochezi na chuki, Kill the Boer aliyoitoa mbele ya hadhara.
Si hayo tu mwaka 2012 alishitakiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo utakatishaji fedha na uhujumu uchumi, mashtaka ambayo mahakama iliamua kuyafuta mwaka 2015 baada ya kuahirishwa mara kadhaa.

Malema ni mfano wa Viongozi wa vyama vya upinzani na wanaharakati ambao hawaambiliki wanaposimama kutetea maslahi ya wananchi amekuwa na msimamo usiotikiswa hata Rais mstaafu Jacob Zuma aliwahi kutabiri kuwa Malema atakuja kuwa Rais wa Afrika Kusini.

Imeandikwa na Peter Mwaihola.
Photo_1747893962635.png
 
Imeandikwa na Peter Mwaihola.View attachment 3341699

Duuh Kwa hiyo malema ni kama TAL!
 
Nasubiri maandishi ya watu fulani humu ambao wao huonaga mzungu or mwarabu kumdhulumu mtu mweusi ni HAKI, mwafrika akitafuta haki yake ni DHAMBI
 
Back
Top Bottom