Hapo utahitaji kulima mazao roho ngumu ambayo hayahitaji uangalizi wa karibu. Mazao hayo yapaswa uvunaji wake ukawa wa mara moja. Mazao hayo ni mengi, km karanga, mahindi, alizeti, mpunga, miwa, viazi vitamu, mihogo na mengine mfano wa haya.
Kamwe usilime mboga mboga na vitu kama migomba maana watavuna haupo na itakula kwako.
Kitu cha kuzingatia hakikisha unakuwepo wakati wa kupanda, kuweka mbolea na wakati wa kuvuna. Usikose kuwepo siku hizo maana wakati wa kupanda mbegu ni pesa zitaliwa kisha watasingizia zilikuwa mbaya hazioti, wakati wa kuweka mbolea, mbolea ni pesa watauza na kudai waliweka mbolea yote nao wanashangaa kwa nini haijafanya kazi labda ilichakachuliwa, wakati wa kuvuna usipokuwepo hapo ndiyo balaaa kabisa maana wanaweza hata kusema japo zao lilisitawi naona tumeibiwa kichawi badala ya kuvuna gunia 100 tumeambua 20 tu.
Weka utaratibu ambao malipo uwe unayafanya wewe. Yaani tafuta watu mkubaliane wafanye kazi malipo unaenda kuwalipa muda mtakaokubaliana. Wahudumu wa shamba wafanye mengine lakini kamwe usiwape jukumu la kulipa pesa. Labda uwe na bahati upate MALAIKA. Mkuu naona na wengine watajazia.