Kilimo cha kisasa cha maembe

Nchi yetu imebarikiwa matunda ya aina nyingi lakini embe ni la kipekee,kwa sababu kuna aina zaidi ya mia moja(100) za maembe, Mi nazijua hizi zifuatazo:

1.Korokocho_Hizi ni ndogo kuliko embe zote zina umbo kama tunda damu,Ila utamu wake kiboko!

2.Sindano_Hizi pia ni ndogo ila zimechongoka kama sindano,na utamu wake hauzidi korokocho.

3.Bolibo_Hizi umbo lake ni la kawaida tu ila zinapendeza hata kuangalia rangi zake,pia tamu ila sio km hizo hapo juu.

4.Fungani_Hizi ni saizi ya kati,ukila km zina nyuzinyuzi ila ni tamu balaa!
 
Bolibo-hili ni embe lisiloiva,ukiona limeiva maana yake limeishaoza,huliwa likiwa na ubichi wake sababu sio chachu kama mengine.

Embe ng'ongo-hili sijui kwanini linaitwa embe mpaka leo, kuanzia muonekano, harufu,ni tofauti na mengine.isipokuwa nalo ni chachu.
 
Embe Mwaka haziivi mtini, ila tamu balaa zinapatikana sana Kilosa na Ifakara,kidodi, kilombero, pia niliziona iringa wanaziuza. Ni nzuri kwa biashara sbb hazibonyei hovyo hovyo alafu tamu sana.
 
Kuna swaoi uwa sipatu majibu labda mnaweza kunisaidia,ni kwa nn unaweza kukuta ndani ya embe kuna mdudu wakati embe hakuna sehem iliyoharibika kwa nje
 
Kwangu namba moja Dodo mbili Zafarani.
 
Kuna embe inaitwa KENTE inakuwa kubwa kama kichwa cha mtoto mchanga, nyingine inaitwa TOMMY. ila sijawahi kuzila nimepanda nasubiri kula.
 
bolibo ndio embe ngumu sana na huwa kubwa na nazipenda kwa sababu ni tam pia nasikia zinapatikana sana zenji..
 
Kaka tunaomba mrejesho. Ulifanikiwa? Aina gani ya embe uliyopata?
Sikufanikiwa kupata maeneo ya hapo Njombe kila niliyewasiliana naye alisema kua inabidi niitoe toka sehemu moja mpaka hapo Njombe.

Amagro walisema niitoe miche kutoka Dar mpaka Njombe kuna mdau aliniambia niwacheki SUA hivyo nitoe miche kutoka Moro mpaka Njombe.

Hao wawili wana kila aina, Amagro walinishauri nichukue Apple au aina fulani mbili hivi zimenitoka jina ndiyi zina soko.
 
Kuna embe kubwa sana naona zinauzwa huku dar 1500 moja
Hivi mbegu yake ipo hapa tz au?
 
Kwa hapa Njombe miche ya miembe niliwai kuiona siku moja tu maeneo ya CRDB au St. Bakita. Jaribu hapo unaweza kuipata. Waulize wale wauza matunda maeneo hayo.
 
Kwa hapa Njombe miche ya miembe niliwai kuiona siku moja tu maeneo ya CRDB au St. Bakita. Jaribu hapo unaweza kuipata. Waulize wale wauza matunda maeneo hayo.
Ahsante mkuu nitafuatilia
 
N Nitawezaje kuwapata hawa KIBITI, niko mbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…