Kilichopo sasa ni utulivu au amani?

mgen

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
22,631
8,417
Wanangu kisu kimefika kwenye mfupa huku USWAZI
Mwisho wa mwezi umepita na sasa kukopa tena Gengeni dukani kumeanza.

Muarubaini ulio jirani umechunwa ngozi kutibu magonjwa arubaini na miti mingine km mjengaua mpera haija salimika. Dawa za hospitali ni stori.

Buku inaachwa nyumbani kwa mamaa asubuhi eti fanya maarifa, ana watoto watatu baba anarudi jioni mikono mitupu naye anadai ubwabwa mboga tatu na chenji akashushie robo gongo

Watoto wamejazana nyumbani kwa baba x wanadai sembe kama baba yao! Na hawakosei muda! wanyime uone utaimbwa Mpaka mkoleni.

Kila kukicha tembele nyanya masalo na dagaa chiliusungu.
Jirani muda mrefu hajala nyama usiku anaota anakula nyama katafuna godoro sio mashara.

Subiri Sasa ukifa kaburi la mshikaki sanda kiroba.
AMANI AU UTULIVU(ffu)?
 
Back
Top Bottom