Kilichobaki ni ushabiki wa vyama tu

Kilichobaki ni ushabiki wa vyama tu

Ja60

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2012
Posts
277
Reaction score
180
Katika uchaguzi huu nionavyo mimi ni kwamba watu wengi hawasikilizi sera za wagombea bali wanashabikia vyama vyao vishinde haijalishi ni nani atashinda kama anatoka chama chake kwake ni burudani ndio maana tunashindana kujaza viwanja vya kufanyia kampeni.
 
Umenena mkuu, ushabiki ka tim za mpira

Kwa mustakabali wa taifa letu siasa haipaswi kufanywa kwa staili ya ushabiki wa mpira haijalishi timu ni mbovu we ni kushabikia tuu.
 
Hapa yanatafutwa mabadiliko tu.Sera,sera kitu gani miaka hamsini yote hizo sera zilikuwa wapi watu ni maskini wa kutupwa.
 
Ni mda wa UKAWA.
Sera hazina tija kwa sasa.
CCM hawajawahi kutekeleza sera zao kikamilifu.
Its a high time to change the course of wind direction
 
Hapa yanatafutwa mabadiliko tu.Sera,sera kitu gani miaka hamsini yote hizo sera zilikuwa wapi watu ni maskini wa kutupwa.

Woga wako ndio umasikini wako wala usisingizie ccm, hao akina Mbowe, Ndesamburo, Lowassa, Sumaye na wengine wengi mlionao huko, hao nao masikini? Punguza ushabiki na mahaba sikiliza wagombea kwa makini, then amua cha kuchagua
 
Lowasa juuuu huyu ndo Rais wetu
 
Mimi nilishaamua hata kabla ya kampeni nitamchagua Lowassa, hivyo mikutano ya kampeni,propaganda za udini au hadithi za Dr wa mihogo hazinibadilishi uamuzi.
 
Hivi kuna ahadi mpya ambapo ukiacha za miaka ishirini iliyopita. sasa kama ahadi ni zilezile kila siku kwa nini kupoteza muda wako kufuatilia kitu kile kile miaka nenda rudi mafanikio hayaonekani. kwa mtu mwenye ufahamu hawezi kufanya hivyo labda kama huyu mtu ni lyapugile kabisa.
 
sioni tofauti za sera za ccm, kama walicha tuahidi maisha bora kwa kila mtanzania wameshidwa na wala hawataki kuirudia kwa maana hawakutimiza hizi sera nyingine za nini? na serikali tuliwapa! kwa watu wenye busara ni bora tuwape UKAWA tuone kama watatimiza ahadi zao
 
Woga wako ndio umasikini wako wala usisingizie ccm, hao akina Mbowe, Ndesamburo, Lowassa, Sumaye na wengine wengi mlionao huko, hao nao masikini? Punguza ushabiki na mahaba sikiliza wagombea kwa makini, then amua cha kuchagua

Siwezi kuchagua wapuuzi waliohujumu mchakato Wa katiba ya wananchi au wale wagonga meza bungeni wanaosubiri kusema ndiyooooo za kishabiki
 
Back
Top Bottom