Luv
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 2,739
- 6,099
Habari wakuu,
Hongereni na majukumu ya kila siku. Kwa mara ya kwanza naomba ushauri humu.
Miaka ya nyuma nilitendwa sana sana kimapenzi, nilikuwa naumia sana, baada ikafika sijui nini kimenitokea kwamba nimezoea au nayachukuliaje mapenzi.
Kila nikiingia kwenye uhusiano ninakuwa nina mawazo ya kufika mbali ila baada ya muda najikuta namchukia yule mtu, sitaki tena kumuona na imekuwa rahisi kwangu kumuacha mtu. Tena namwambia sikutaki tuachane baada ya kuona nakufanyia visa huelewi.
Nikishakaa peke yangu nakuwa nafurahia kwa muda then napatwa na upweke sana. Ila nikiwa kwenye mahusiano mambo ni yale yale nayarudia.
Napenda kuona mtu analia kwa ajili yangu nakuwa nafurahi sana moyo wangu unakuwa na amani. Na bahati nzuri au mbaya unakuta kweli mtu analia sana jinsi navyofanya vituko, naulizwa kama anahitajika kujirekebisha ila namwambia naona bora tuachane?
1. Siipendi hii hali kutoka moyoni ila huwa inanijia automatically.
2. Natamani kubadilika niwe mwema kama zamani ila kila nikijaribu nashindwa.
3. Naona huruma baada ya mtu kumfanyia matendo mabaya ila siwezi tena kumrudisha (nakuwa na kauli sio nzuri, kukaripia, kukutafutia makosa hasa ya kuchepuka ni kawaida)
Mnisaidie nifanyaje ili niondokane na hii hali ukizingatia jioni bado kidogo kufika.