Kila kukicha ugomvi katika "ndoa nyingi" unaongezeka, kisa wivu.
Mwanaume hamuamini mwanamke ilhali naye anacheat, upande ule mwanamke hamuamini mwanaume kisa anahisi anacheat.
Ukweli ni kuwa mwanaume hataacha kutamani mwanamke yoyote mwenye mvuto mpaka dunia itakapokoma kuwapo. Na mwanamke hatokubali kuvumilia kushare mapenzi na mwanamke mwenzie, naye hatoacha kupenda na kutamani mwanaume yeyote mwenye mvuto mpaka dunia itakapokoma kuwapo.
Kila mtu afanye vile anavyoufurahisha moyo wake, full stop, ukichoshwa na mwenzio piga chini tafuta anaekusuuza moyo wako.
Ya nini tunabanana wakati hatuaminiani? Tunamdanganya nani kuwa hatuna ugomvi ndani ya nyumba zetu wakati ukweli ni kuwa hatuna amani.
Hii sio sheria na wala sitaki mnishambulie, mie nimefunguka tu, mchana mwema, tutaonana jioni.
Mtendahaki