Na tanzania ni nchi ya ngapi kiuchumi Afrika ? Au imepanda/imeporomoka mpaka kuwa ya ngapi kiuchumi ?
Je mfumuko wa bei umeshuka kwa asilimia ngapi ?Au je ni nchi ya ngapi kwa kudhibiti rushwa ?thamani ya pesa ikoje ,hali ya maisha ya wananchi wake nikiwemo mimi na wewe ,majomba,wapwa na wajukuu zetu zikoje,wanakwenda choo mara ngapi kwa wiki ?wakiugua
wanachimba mizizi au wanatibiwa hospitali.
Waambie watupe taarifa kwa maswali hayo hapo juu.
Kwani hamjui na hao wanaofanya tafiti wanaandika ili na wao wakalambe miguu ya hao jamaa. Sasa mbona na mshikaji wake wa Bondeni hamshangai amepataje wa sita sijui wakati kila kosa mbaka na kubaka analo. Nyie bwana acheni utani huyu mjamaa ni wa mwisho tu ila tu appearance labda mpaka na watafiti wanakoshwa nalo. Angekuwa Slaa hapa mpaka namba mbili au mmoja angeshika kwa performance yake
Sina shaka na JK kuwa wa 10 katika bara ambalo una marais kama akina Bhagbo, Kibaki, Mgabe, Zenawi, Al Bashir, n.k. Maana hata ukienda katika shule zile ambazo hazijawahi kutoa hata mtoto mmoja kwenda sekondari tangu zianze, lazima wa kwanza, wa pili, wa tatu na wa mwisho utawapata KWA MAANA unaweza kuwa wa kwanza katika kundi la wabovu ila huyo wa mwisho kwenye kundi bovu ni balaa!
Wangesema JK ni 100 kwa ubora Duniani hapo ningechanganyikiwa lakini kuwa wa 10 Afrika sina tatizo kwa vile inafahamika kabisa kuwa Marais wazuri katika maana ya uongozi wenye upeo na dhamira njema katika Afrika hawawezi kuzidi 5.
Anastahili jamani,tusikatae sababu ya itikadi,ushabiki na mzugo wa kisiasa.
again ANTIJAKAYA DISEASE
Nionyeshe wizi mmoja alioufanya Kikwete!