UKAWA nao! Yaani mtego uko dhahiri nao wanakubali kukaa na Kikwete na Cheyo (ambaye bado anakula posho ya BMK) na kutangaza kukubaliana kuahirisha BMK??? Halafu "wanakubaliana" na Kikwete (sio sehemu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano) kuifanyia mabadiliko Katiba ya sasa? Eti matokeo ya urais yahojiwe mahakamani, Rais ashinde kwa 50%+1, Tume Huru ya Uchaguzi? Nani watajadili na kupitisha mapendekezo haya? Sio Kikwete! Ni Sitta, Membe, Lowassa, Makamba, Wasira Ngeleja - unawajua wote na maslahi yao ktk uchaguzi ujao. Kweli? UKAWA wameingizwa tena mjini!!