Ccm ndo ilimuibua magufuliMkapa ndio aliomuibua magufuli.
Jitoe gamba utaelewa Kitochoendelea Dodoma....ila ukibaki Na gamba utakaa uelewe kamwe...Sasa wewe unashangaa uwezo wa JK kisiasa?
Huyu mtu kafundisha Siasa Jeshini
Akiwa bado kijana wakati huo amepangiwa Zanzibar kufanya kazi za chama alikuwa Instrumental kwenye kuitransform ASP ya Zanzibar kuwa CCM.
Huyu mtu alimuumiza kichwa Mwalimu Nyerere pale alipombwaga Mkapa kwenye kumtafuta mgombea wa CCM kwa nafasi ya Uraisi mwaka 1995, pamoja na Rafu na Figisu zote alizofanyiwa alijishusha, akatumikia serikali na baadae akaibuka kidedea mwaka 2005.
JK ni "mtoto" wa mjini, kakulia Dar es salaam, maskani yake Saigoni, Karuka debe la mjini, kiufupi ni mjanja ndiyo maana alikuwa akisema, Usiwe kama mbayuwayu, za Kuambiwa Changanya na za kwako.
Pia hulka yake ni ya kibinadamu sana, anapenda watu, kila uamuzi wake anafikiria kuhusu mustakbali wa wenziwe, JK siyo mkurupukaji, ni mkimya lakini ni master strategist
Sasa kama ni mwanasiasa wa karne alishindwa vipi kuishawishi Nec impigie kura mdogo wake bwana Membe ambaye ndio lilikuwa chaguo lake?Nadeclare interest mapema sina chama....
Watanzania wengi tumekuwa wasahaulifu sana na hilo wakati mwingine hutugharimu. Hakuna wakati (bila Mwalimu) mgumu wa sekeseke, wa pasua kichwa ambao CCM imepitia kama kipindi cha Lowasa. Katika kipindi hiki watu walikuwa hawalali, wengine wanalala milango wazi, wengine hawabanduki humu JF, hawazimi redio wala tv wakisubiri kusikia CCM imesambaratika.
Huyu mstaafu mimi namkubali sana, maana anauwezo wa kugeuza upepo katika namna ambayo watu hawatarajii. Hebu wewe mwenyewe fikiria, NEC nzima ilijipanga ikapangika kumtetea Lowasa, dakika tano tu baada ya mstaafu kuingia zilimtosha kuisambaratisha kambi ya jamaa vipande vipande na kisha kumchinjia baharini mtarajiwa wao na kumuibua JPM.
Wakati wa namna hii umewadia tena, naona wakina Mbowe, Zitto, Mashinji na jamii yao hawalali, wengine wanalala milango wazi, wengine hawabanduki humu JF, hawazimi redion wala tv wakisubiri kusikia CCM imesambaratika. Kwa jinsi navyofahamu uwezo wa mstaafu kisiasa hara kama akiamua kutokumkabidhi JPM kijiti nina uhakika CCM haiwezi meguka kama wengine wanavyodhani...
Watanzania ndio tulimwibua MagufuliCcm ndo ilimuibua magufuli
Chaguo la kikwete lilikuwa Membe kule Dodoma alienda na majina mfukoni lakini wafuasi wa lowasa walipoona kawakomoa na wao wakaamua kumkomesha kwa kumpigia kura Magufuli.Watanzania ndio tulimwibua Magufuli
Huyo mtoto wa juzi hawezi kuwajua akina Njelu Kisaka.Kuweka kumbukumbu sahihi. Wakati mgumu zaidi CCM kupitia ilikuwa ni 1993-4 wakati wa sekeseke la G55. Kumbuka ni wabunge wa chama kimoja wakiipeleka puta serikali kuhusiana na suala la serikali ya Tanganyika. Hili la Lowassa nalo lilikuwa jambajamba ya kutosha lakini si kubwa kuliko G55.
aliyeingia na majina matano ukumbini ni nanMkapa ndio aliomuibua magufuli.
Wala hawezi kuwajua kina Tuntemeke Sanga. Hawezi jua hadi Mwalimu alilazimika kuandika kitabu cha Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania ambacho kilikataliwa kuchapwa humu Tanzania hadi akaenda kukichapia Zimbabwe.Huyo mtoto wa juzi hawezi kuwajua akina Njelu Kisaka.
Wala hajui kwanini Malecela aling'oka kwenye nafasi ya Waziri Mkuu.
Na pengine hajui kwanini Kolimba alipotezwa. G55 ilitikisa bhana.
Ccm ni wale waliokua wanaimba... tuna imanii na LowasaaCcm ndo ilimuibua magufuli