Kikwete mwanasiasa wa karne: Kama aliweza kucheza muziki wa Lowassa, wa Magufuli ni cha mtoto

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,478
2,301
Nadeclare interest mapema sina chama....

Watanzania wengi tumekuwa wasahaulifu sana na hilo wakati mwingine hutugharimu. Hakuna wakati (bila Mwalimu) mgumu wa sekeseke, wa pasua kichwa ambao CCM imepitia kama kipindi cha Lowasa. Katika kipindi hiki watu walikuwa hawalali, wengine wanalala milango wazi, wengine hawabanduki humu JF, hawazimi redio wala tv wakisubiri kusikia CCM imesambaratika.

Huyu mstaafu mimi namkubali sana, maana anauwezo wa kugeuza upepo katika namna ambayo watu hawatarajii. Hebu wewe mwenyewe fikiria, NEC nzima ilijipanga ikapangika kumtetea Lowasa, dakika tano tu baada ya mstaafu kuingia zilimtosha kuisambaratisha kambi ya jamaa vipande vipande na kisha kumchinjia baharini mtarajiwa wao na kumuibua JPM.

Wakati wa namna hii umewadia tena, naona wakina Mbowe, Zitto, Mashinji na jamii yao hawalali, wengine wanalala milango wazi, wengine hawabanduki humu JF, hawazimi redion wala tv wakisubiri kusikia CCM imesambaratika. Kwa jinsi navyofahamu uwezo wa mstaafu kisiasa hara kama akiamua kutokumkabidhi JPM kijiti nina uhakika CCM haiwezi meguka kama wengine wanavyodhani...
 
Sasa wewe unashangaa uwezo wa JK kisiasa?

Huyu mtu kafundisha Siasa Jeshini

Akiwa bado kijana wakati huo amepangiwa Zanzibar kufanya kazi za chama alikuwa Instrumental kwenye kuitransform ASP ya Zanzibar kuwa CCM.

Huyu mtu alimuumiza kichwa Mwalimu Nyerere pale alipombwaga Mkapa kwenye kumtafuta mgombea wa CCM kwa nafasi ya Uraisi mwaka 1995, pamoja na Rafu na Figisu zote alizofanyiwa alijishusha, akatumikia serikali na baadae akaibuka kidedea mwaka 2005.

JK ni "mtoto" wa mjini, kakulia Dar es salaam, maskani yake Saigoni, Karuka debe la mjini, kiufupi ni mjanja ndiyo maana alikuwa akisema, Usiwe kama mbayuwayu, za Kuambiwa Changanya na za kwako.

Pia hulka yake ni ya kibinadamu sana, anapenda watu, kila uamuzi wake anafikiria kuhusu mustakbali wa wenziwe, JK siyo mkurupukaji, ni mkimya lakini ni master strategist
 
Unaweza kumsifia sana jk kuwa ndo aliokoa jahazi...ila inawezekana kabisa kuwa hata yeye mweyewe alicheza tu ngoma ambayo wala mpigaji hakumjua...ni watu wachache sana wanaweza kuelewa hili ila nakuambia ule mziki jk angeachiwa peke yake sasa hv tungekuwa tunaongea habari nyingine Kabisa...kila mmoja hata wewe unajua kabisa jk alikuwa amelalia wapi 100% usitake kujitoa akili...na endapo wazee wasingecheza Na akili yake bila yeye kujua Leo tungekuwa tunaongea mengine Kabisa...ni hayo tu kwa sasa
 
Sasa wewe unashangaa uwezo wa JK kisiasa?

Huyu mtu kafundisha Siasa Jeshini

Akiwa bado kijana wakati huo amepangiwa Zanzibar kufanya kazi za chama alikuwa Instrumental kwenye kuitransform ASP ya Zanzibar kuwa CCM.

Huyu mtu alimuumiza kichwa Mwalimu Nyerere pale alipombwaga Mkapa kwenye kumtafuta mgombea wa CCM kwa nafasi ya Uraisi mwaka 1995, pamoja na Rafu na Figisu zote alizofanyiwa alijishusha, akatumikia serikali na baadae akaibuka kidedea mwaka 2005.

JK ni "mtoto" wa mjini, kakulia Dar es salaam, maskani yake Saigoni, Karuka debe la mjini, kiufupi ni mjanja ndiyo maana alikuwa akisema, Usiwe kama mbayuwayu, za Kuambiwa Changanya na za kwako.

Pia hulka yake ni ya kibinadamu sana, anapenda watu, kila uamuzi wake anafikiria kuhusu mustakbali wa wenziwe, JK siyo mkurupukaji, ni mkimya lakini ni master strategist
Jitoe gamba utaelewa Kitochoendelea Dodoma....ila ukibaki Na gamba utakaa uelewe kamwe...
 
Nadeclare interest mapema sina chama....

Watanzania wengi tumekuwa wasahaulifu sana na hilo wakati mwingine hutugharimu. Hakuna wakati (bila Mwalimu) mgumu wa sekeseke, wa pasua kichwa ambao CCM imepitia kama kipindi cha Lowasa. Katika kipindi hiki watu walikuwa hawalali, wengine wanalala milango wazi, wengine hawabanduki humu JF, hawazimi redio wala tv wakisubiri kusikia CCM imesambaratika.

Huyu mstaafu mimi namkubali sana, maana anauwezo wa kugeuza upepo katika namna ambayo watu hawatarajii. Hebu wewe mwenyewe fikiria, NEC nzima ilijipanga ikapangika kumtetea Lowasa, dakika tano tu baada ya mstaafu kuingia zilimtosha kuisambaratisha kambi ya jamaa vipande vipande na kisha kumchinjia baharini mtarajiwa wao na kumuibua JPM.

Wakati wa namna hii umewadia tena, naona wakina Mbowe, Zitto, Mashinji na jamii yao hawalali, wengine wanalala milango wazi, wengine hawabanduki humu JF, hawazimi redion wala tv wakisubiri kusikia CCM imesambaratika. Kwa jinsi navyofahamu uwezo wa mstaafu kisiasa hara kama akiamua kutokumkabidhi JPM kijiti nina uhakika CCM haiwezi meguka kama wengine wanavyodhani...
Sasa kama ni mwanasiasa wa karne alishindwa vipi kuishawishi Nec impigie kura mdogo wake bwana Membe ambaye ndio lilikuwa chaguo lake?

Wewe huoni kwamba hapa Lowasa ndio alionesha umwamba? Au nyinyi mnayachambuwa vipi matukio? Ni Lowasa huyu huyu ndio amefanya sasa ikulu ya Magufuli iko chini ya mikono salama ya UKAWA.
 
Namheshimu sana JK, kwanza ni mtu ambaye hakurupuki kwenye maamuzi yake na ni mtu ambaye huwa anasubira na anyependa kukisoma kitu kabla ya kufanya maamuzi ili kujipa muda wa kutosha kufanya maamuzi. Lakini mtoa mada huenda hukuelewa nani alimuibua Ngosha na huenda hukujua nani aliekuwa engineer kwenye suala la Laigwani kutoswa na hapo ndipo ulipoharibia bandiko lako. Kama kitu hukijui huna sababu za kukisema kwani huwa kinakufanya unaonekana sio mfuatliaji wa mambo na kila unapopost kitu hata kama ni cha maana watu hawatakisoma tena kwa kuwa wanakuona huju kitu na utawapotezea muda. Kwa taarifa aliekuwa kinara wa kumuibua Ngosha alikuwa chinga na aliekuwa kinara wa kumuangamiza laigwani alikuwa huyohuyo kumbuka jina la laigwani lilikatiwa kwenye kamati ya maadili ambayo enjinia alikuwa chinga. Japo JK nae alikuwa kwenye hizo harakati ila alikuwa hana ramani ya kufanikisha kwani alikuwa mwoga wa madhara na jamaa ni mtu wa kupima sana.
 
Kuweka kumbukumbu sahihi. Wakati mgumu zaidi CCM kupitia ilikuwa ni 1993-4 wakati wa sekeseke la G55. Kumbuka ni wabunge wa chama kimoja wakiipeleka puta serikali kuhusiana na suala la serikali ya Tanganyika. Hili la Lowassa nalo lilikuwa jambajamba ya kutosha lakini si kubwa kuliko G55.
 
Huyo mtoto wa juzi hawezi kuwajua akina Njelu Kisaka.

Wala hajui kwanini Malecela aling'oka kwenye nafasi ya Waziri Mkuu.

Na pengine hajui kwanini Kolimba alipotezwa. G55 ilitikisa bhana.
 
Wala hawezi kuwajua kina Tuntemeke Sanga. Hawezi jua hadi Mwalimu alilazimika kuandika kitabu cha Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania ambacho kilikataliwa kuchapwa humu Tanzania hadi akaenda kukichapia Zimbabwe.
 
Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom