Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,114
- 34,958
MOJA ya sifa kuu za jeshi lolote lile duniani ni nidhamu, bila nidhamu ya kweli miongoni mwa askari na maofisa, basi jeshi husika hugeuka na kuwa genge la wahuni. Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri miaka kadhaa iliyopita katika nchi jirani ya Uganda, Rais Yoweri Museveni, alimteua Meja Jenerali Kale Kayihura, kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo.
Hatua hiyo ilitokana na jeshi hilo kupoteza hadhi na heshima mbele ya umma baada ya kukithiri kwa vitendo vya uonevu dhidi ya raia, rushwa, ukiukwaji wa maadili ya kazi ya polisi na dhambi nyingine nyingi.
Wakati Meja Jenerali huyo anateuliwa, hakuwa askari polisi, bali alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Jeshi la Wananchi la Uganda (UPDF), na hadi sasa bado anaendelea na wadhifa huo nyeti.
Kusema kweli bila kungata maneno, Jeshi la Polisi Tanzania limepoteza hadhi na heshima mbele ya jamii yetu kwa kiasi kikubwa sana, na hakuna hatua zozote zile zenye dhamira ya kweli zinazoonekana kuchukuliwa kurekebisha hali hiyo.
Kama isingekuwa kazi iliyotukuka inayofanywa na vyombo vya habari nchini, bila shaka hali ingekuwa mbaya zaidi, lakini vyombo vya habari vimesaidia kuweka hadharani dhambi za polisi, hata pale polisi wanapoamua kusema uongo, mathalan katika tukio la kupigwa risasi mwanahabari Shaaban Matutu, Desemba 4, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ukiukwaji wa haki za binadamu unaoambatana na mauaji yanayofahamika na yasiyofahamika ya raia wasio na hatia na hata wenye hatia kwa pamoja, vimelifanya Jeshi la Polisi kuwa chombo kisichoaminika tena mbele ya Watanzania, hasa wale masikini ambao ndio wengi.
Kuthibitisha hili, hebu Serikali iandae utaratibu wa kura za maoni miongoni mwa Watanzania ili kubaini imani ya wananchi na jeshi hilo, bila shaka zaidi ya asilimia 90 watasema hawana imani na polisi.
Katika kuthibitisha hilo ndani ya muda usiozidi wiki mbili, viongozi wawili wanaoheshimika kabisa katika jamii ya Watanzania wametamka bayana kuwa jeshi hilo linakiuka misingi ya haki za binadamu.
Si lengo kurudia kile walichokisema viongozi hao, lakini hapa nawazungumzia Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza Mzalendo, Jaji Mark Bomani, ambao wote walizungumzia ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na polisi.
Ukiacha viongozi hao wawili, hata Mkuu wa nchi, Rais Jakaya Kikwete, wakati akihutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wiki kadhaa zilizopita mjini Dodoma, alionyesha kutofurahishwa na vitendo vya polisi.
Ila kwa sababu hakuwa anazungumza na polisi, bali wanachama wa CCM, aliwaambia waache kuwatumia polisi katika kukabiliana na hoja za wapinzani, badala yake wapambane na wapinzani kwa hoja si kwa kutumia polisi.
Kwa lugha rahisi, Rais Kikwete aliliambia Jeshi la Polisi kuwa wakati umefika sasa liache kutumiwa na makada na viongozi wa CCM kunyanyasa wananchi kwa sababu ya tofauti za kiitikadi.
Kauli hiyo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ilikuja baada ya vilio vilivyodumu kwa miaka mingi kutoka kwa wananchi wakilaumu jeshi hilo kuwa linatumiwa na chama tawala kuvikandamiza vyama vya upinzani, jambo ambalo viongozi wa Jeshi la Polisi wamekuwa wakilipinga bila soni, ilhali hata mtoto mdogo anaweza kuthibitisha hilo.
Tabia hiyo ya polisi kutumiwa na wanasiasa wa chama tawala sio tu imekuwa ikizuia ukuaji wa demokrasia nchini kama chachu ya maendeleo, lakini imesababisha wananchi kupoteza maisha mara kadha wa kadha bila hatua zozote kuchukuliwa, zaidi ya kuambiwa mauaji yanachunguzwa.
Polisi wetu wanaua raia, kwa mfano, kwa mujibu wa vyombo vya habari, kauli iliyotolewa na wauguzi wa Hospitali ya Mwananyamala baada ya kumpokea mwanahabari Matutu, kwa kweli ilikuwa ya kutisha na kuhuzunisha.
Nanukuu moja ya magazeti ya kila siku yaliyomnukuu mwandishi Matutu; Tukiwa pale huku maaskari wakiwazuia baadhi ya wafanyakazi waliofika kuniona wasipige picha, askari walijaribu kila mbinu kunishawishi nisifungue malalamiko dhidi yao na ndipo manesi waliokuwa eneo hilo waliniambia nina bahati kwa vile nimeletwa nikiwa hai.
Hapa tunaletewa watu wakiwa hoi au wamekufa na wanatupwa hapa kisha askari wanaondoka halafu kesho unasikia majambazi wameuawa kwa risasi wakipambana na polisi.
Ni nini maana ya nukuu hii? Maana yake ni kuwa manesi na wauguzi wa Hospitali ya Mwananyama na kwingineko wana shuhuda nyingi sana za unyama unaofanywa na Jeshi la Polisi yakiwamo mauaji, jeshi ambalo lilipaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.
Ukiacha raia kuuawa na kupigwa wanapokuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi, lakini pia polisi wana sifa nyingine mbaya kabisa, nayo ni kuwapora fedha na vitu vingine watuhumiwa.
Mmoja wa mashuhuda wa hili ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye miaka ya nyuma aliwahi kukamatwa kwenye vurugu za kisiasa, akapigwa na kuumizwa mkono wa kulia kama sijasahau na sehemu nyingine za mwili, baadaye aliwekwa katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Baada ya Profesa Lipumba kuachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitamka hadharani kuwa askari polisi wetu ni wezi, kwa sababu wakati wa kumkamata walimwibia saa na fedha alizokuwa nazo kwenye mifuko ya suruali yake. Sikumbuki kama polisi walikanusha madai hayo.
Mifano ya polisi kuwapora raia mali zao ni mingi, lakini nimetoa mfano wa tukio la kukamatwa Profesa Lipumba ambalo ni la siku nyingi, ili kuonyesha vitendo hivyo havikuanza leo ndani ya jeshi hilo, bali sasa vimeota mizizi.
Tukiacha mauaji, unyanyasaji wa aina nyinginezo na vipigo, pia jeshi letu hilo lina sifa nyingine mbaya kabisa, ya kuwabambikizia kesi za ujambazi wa kutumia silaha na mauaji watuhumiwa wa makosa mbalimbali, pamoja na raia wasiokuwa na hatia.
Hili la kubambikizia kesi za ujambazi wa kutumia silaha na mauaji wananchi halina ubishi wowote, Serikali iunde tume huru itembelee magereza ya mahabusu hasa ya mijini ambako kuna polisi wajanja (watoto wa mjini), kisha watuhumiwa wa mauaji na ujambazi wahojiwe mmoja mmoja.
Naamini siku tume hiyo itakapotoa ripoti yake, Watanzania na wapenda haki ndani na nje watafahamu ukubwa wa tatizo hilo ambalo linafumbiwa macho, kwa sababu waathirika wakubwa wa tabia hiyo ya polisi ni watoto wa masikini wanaokaa Tandale kwa Mtogole, Dar es Salaam na maeneo yanayofanana na hayo katika sehemu nyingine za nchi yetu.
Hayo yote yanadhihirisha jambo moja kubwa, nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi imeshuka sana sana, na hilo linachangiwa na jeshi kuwa na uongozi dhaifu uliokosa mashiko ndani ya chombo hicho.
Pia hali hiyo inatokana na usaili wa askari polisi kufanywa kinyume cha taratibu, na Watanzania kujikuta tuna baadhi ya askari polisi wasiokuwa na maadili wala sifa ya kufanya kazi ya polisi. Ndio sababu polisi wengi wameingia jeshini kwa kutumia vyeti feki, hili si suala dogo, athari zake ni kubwa mno mbele ya safari.
Kwa sababu kuna uwezekano wahalifu wengi tu ambao wengine hawakuweza hata kumaliza shule, wameingia ndani ya Jeshi la Polisi kwa kutumia vyeti vya ndugu au rafiki zao, na matokeo yake ni tabia za ajabu tunazoziona miongoni mwa askari na maofisa wa polisi.
Kwa nini nimetoa mfano wa Rais Museveni kumteua Meja Jenerali Kayihura wa Uganda mwanzoni mwa makala haya, ni kwa sababu Jeshi la Polisi Tanzania linatakiwa kusukwa upya na nidhamu kurejeshwa na kusimamiwa.
Si jambo rahisi kwa Mkuu wa Jeshi hilo IGP Said Mwema, kuweza kuleta mabadiliko ndani ya jeshi hilo kutokana na sababu nyingi tu ambazo nyingine hatuwezi kuziandika kwa sasa.
Rais Kikwete kama kuna kitu Watanzania watakukumbuka pamoja na mema na mazuri yote uliyoifanyika Tanzania katika kipindi cha utawala wako, basi ni kuwaachia Jeshi la Polisi lenye nidhamu, maadili, kutenda haki na kulinda kwa dhati raia na mali zao.
Wahenga walisema; Samaki mmoja akioza, basi wameoza wote, kwa sababu hiyo, kama utaona vema tafuta Mkuu wa jeshi hilo nje ya Jeshi la Polisi, mpe kazi ya kulinyoosha, na kwa kufanya hivyo (narudia), Rais Kikwete Watanzania watakukumbuka, kwa sababu ni hakika wamechoshwa na vitendo vya maofisa na askari polisi.
Kama umeweza kuteua maofisa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kusimamia asasi nyeti serikalini na zimekuwa na mafanikio na nidhamu, kwa nini usifanye hivyo kwa Jeshi la Polisi?
Wakati umefika sasa, mpumzishe IGP Mwema, alipwe mafao yake akapumzike nyumbani kwake iwe Dar es Salaam au Moshi mkoani Kilimanjaro, kisha teua Jenerali mmoja makini asiye na chembe ya mzaha katika utendaji kazi akarekebishe Jeshi la Polisi. Utakumbukwa kwa hilo.http://www.rai.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=159:kikwete-mpumzishe-igp-mwema&catid=28:jamii&Itemid=39