Jitahada za Rais wa awamu ya nne na serikali yake katika kukiimarisha chama cha mapinduzi tangu akiwa waziri mpaka urais.
Huyu ni Bwana Jakaya M. Kikwete ni kiongozi ambaye ameweza kujitengenezea mazingira mazuri kabla ya kuwania nafasi ya urais tangu akiwa bado ni waziri wa mambo ya nje. Huyu bwana aliweza kuwashawishi vijana wengi na kuwapata wanachama wengi kabla ya kupata uongozi wa urais, alitumia muda wa ziada katika kuwasikiliza shida zao na maoni pia, hata kama alikosa muda wa kufanya mazungumzo katokana na kuwa na kazi nyingi alipanga siku maalumu ya kuwasikiliza watu mbali mbali ikiwemo kuwashawishi mpaka alipopata nafasi ya kugombea nafasi ya urais kuanzia kwa njia ya maoni mpaka urais wenyewe na kufanikiwa kupata ushindi wa kishindo.
Cha ajabu na kushangaza baadhi ya mawaziri wake waliowateuwa hatakufuata nyayo zake zaidi ya kuweka maslahi yao mbele kuliko maslahi ya chama chenyewe hii imeshababisha chama kuyumba na wanachama wengi kuhamia vyama pinzani na chama kuporomoka. Matokeo yake ni kumtupia lawama na kudai anakiuwa chama lakini hili si kweli bali ni baadhi ya mawaziri wasio waadhilifu katika utendaji wao wa kazi, kwa sasa inalazimika baadhi ya viongozi wa CCM kutumia nguvu ya ziada ili kukirejesha chama katika hali ya kawaida baada ya chama kuanza kuporomoka.
Katika viongozi walijaribu kumuenzi Baba wa Taifa hili hayati Mw/Nyerere ni Jakaya Kikwete na sivinginevyo. Imefika wakati chama kimekuwa na matabaka hii inaonyesha jinsi gani viongozi wetu wasivyo waadilifu bali wako kwa maslahi yao ni sio chama chenyewe au wananchi waliowaweka madarakani. Ili kukinusuru chama hiki kisiendelee kupoteza muelekeo unatakiwa ushawishi mkubwa kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa hili, hii ikiwepo kupewa kipaumbele katika mambo muhimu kama Elimu. Ujasiriamali na Ajira zote kwa ujumla, kwa mfano vijana wengi wamejiajiri wenyewe lakini wanasumbuliwa na mgambo wa jiji hii inachangia vijana kukichukia chama na kuhamia vyama vingine, ikiwemo ongezeko la uhalifu nchini kutokana na ukosefu wa ajira.
Lengo la waraka huu nikuomba Appointment ya kuonana na Mhe. Rais na kuomba ushauri wa kukiimarisha chama.