kamanda wa anga
Member
- Apr 7, 2012
- 47
- 55
baba yako ndo anajua maana ya urais?
Tangu aingie madarakani jk ameshimdwa kuongoza nchi kwa sababu:
1.watu anaowateua wote ni washikaji hivo kila waziri na wakurugenzi wanafanya wanavotaka bila kumuogopa.
2.Amekuwa kama mzazi anayewapangia kazi watoto kazi wafanye na hachukui hatua yoyote wasipofanya.
3.Haoneshi dhamira ya dhati kwani serikali yake haina mipango maalumu inayoeleweka. Mfano, bajeti ya 2011/2012 waliahidi ajira elfu 60 lkn sijui hiyo hoja imeenda wapi na mwaka wa fedha umeisha.
4.Safari za nje ni nyingi mno kana kwamba ikulu kuna kunguni. Aige mfano wa Paul Kagame wa rwanda!
5.Amekuwa mtu wa maneno mno kuliko vitendo, mara ari mpya,kasi mpya na nguvu ya ajabu, kilimo kwanza, maisha bora kwa kila mtanzania, tanzania bila ukimwi inawezekana,
6.Waziri mkuu wake ni kama kituko cha karne! Hakuwahi kuonesha chochote cha maana tangu ateuliwe. Mda wote ni mtu wa kulalamika na kulaani.
Historia itawahukumu maana kila waziri, makatibu wakuu, wakurugenzi na wengine wanaiba kwa kasi mpya ili 2015 wakastaafu salama. Watanzania msitegemee chochote mda uliobaki. Jiandae kwa hali ngumu zaidi!
Kulia hakumaanishi kuguswa na Jambo, unaweza kulia kwa kujoki. Kama ni suala la kulia iweje Waziri Mkuu atupiwe lawama kuwa hawajibiki wakati tatizo la mauaji ya Albino lilimgusa hadi chozi likamdondoka?Amekuwa ni mtu wa kucheka mno. kucheka kumezidi, hata siku ile analaani mauwaji ya albino alikuwa anacheka tu baada ya kukasilika sana aonekane vitendo hivyo vinamwuzi
Naamini jk naye atakuwa sio mwaminifu, kivipi??
--kwani haiwezekani mtu ukampa kazi mtu ambaye cag amemprove kuwa ni mwizi na ukasuasua kumchukulia hatua, mazingira aya yamejaa shaka dhidi ya mkuu wa kaya na ni wazi hata yeye alofanya uteuzi huo sio mwaminifu hata
Mkapa aliwahi kuuliza hivi "Kwani Kikwete ni robot"?
kwa baba yake ni rais?
Huna sababu ya kupigwa ban mkuu, Mods walishakujua kuwa wewe ni pumba man.Niliwahi kupigwa ban niliposema uongozi wa Jk hauna tofauti na wa Juha.
Japo sitasema hivyo tena, huo ndio uhalisia
Huna sababu ya kupigwa ban mkuu, Mods walishakujua kuwa wewe ni pumba man.
Huwezi tambua hilo mkuu kwa sababu na wewe ni mmojawapo wa wanaonufaika na mfumo wa sasa wa hii serikali ya JK. Kweli shibe mwana malevya na njaa mwana malegeza. Kama unafikia kuona ni kweli serikali imewafanyia kitu kikubwa watanzania basi umepofuliwa macho hadi roho yako. Eeeeh mwenyezimungu angamiza hiki kizazi kinachokandamiza wanyonge. Tunaweka ktk mikono yako hawa wahalifu na wanyonyaji wa uchumi wetu.Mbona hueleweki hayo uliyoyasema yana uhusiano gani na thread yako? Istoshe naona uko kimajungu zaidi. Unazo takwimu zinazoonesha kwamba mpaka sasa hakuna watu walioajiriwa na kuonesha kuwa hadi Rais anamaliza muda wake atakuwa hajatimiza ahadi zake? Huwzi kufananisha Tanzania na Rwanda hasa katika suala zima za mahusiano ya kimataifa na mifumo ya kiutawala. Ukumbuke kwamba Rwanda mara nyingi ilikuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe hivyo inawezekana kabisa Rwanda wasiwe na mahusiano mazuri na nchi nyingine, na mfano mwingine wa Rwanda ni Zimbabwe.
Kuhusu nia ya dhati ya serikali ya JK mimi kwa upande wangu naona kama nia wanayo ila kuna vikundi vya watu wachache ambao wapo kwa ajili kuupotosha umma kuwa Serikali haifanyi kitu. Watu hao ni kama wewe mwandishi wa hii Thread na ndiyo maana hata ulichokiandika kinaonesha wazi ni majungu, wapo wanasiasa na mafisadi waliotoswa nao wapo kwa ajili ya kuibeza Serikali ilioko madarakani. Kwa mtindo huo wa propaganda juhudi za Serikali haziwezi kuonekana kwani ni sawa na kuchota maji kwa kijiko na kuyamwaga baharini.
Mbona hueleweki hayo uliyoyasema yana uhusiano gani na thread yako? Istoshe naona uko kimajungu zaidi. Unazo takwimu zinazoonesha kwamba mpaka sasa hakuna watu walioajiriwa na kuonesha kuwa hadi Rais anamaliza muda wake atakuwa hajatimiza ahadi zake? Huwzi kufananisha Tanzania na Rwanda hasa katika suala zima za mahusiano ya kimataifa na mifumo ya kiutawala. Ukumbuke kwamba Rwanda mara nyingi ilikuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe hivyo inawezekana kabisa Rwanda wasiwe na mahusiano mazuri na nchi nyingine, na mfano mwingine wa Rwanda ni Zimbabwe.
Kuhusu nia ya dhati ya serikali ya JK mimi kwa upande wangu naona kama nia wanayo ila kuna vikundi vya watu wachache ambao wapo kwa ajili kuupotosha umma kuwa Serikali haifanyi kitu. Watu hao ni kama wewe mwandishi wa hii Thread na ndiyo maana hata ulichokiandika kinaonesha wazi ni majungu, wapo wanasiasa na mafisadi waliotoswa nao wapo kwa ajili ya kuibeza Serikali ilioko madarakani. Kwa mtindo huo wa propaganda juhudi za Serikali haziwezi kuonekana kwani ni sawa na kuchota maji kwa kijiko na kuyamwaga baharini.