Wapinzani wana hoja nyingi na nzuri tu za kuiondoa CCM madarakani. Wakitengeneza documentaries za mambo kama haya wakayatolea maelezo mazuri Watanzania watawaelewa kuliko kila kukicha wanaanzisha vyama vipya. Zipo shule za msingi mbavu za mbwa, mahakama za mwanzo magofu, vituo vya polisi majalala, barabara za vijijini mahandaki, mazao ya wakulima yasiyo na soko, ukosefu mkubwa wa ajira, uhaba wa walimu mashuleni, sekondari zisizo na maabara wala maktaba,........