fdizzle
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 1,900
- 2,394
Uchaguzi mkuu wa Tanzania kwa mwaka 2015 ulikuwa na agenda kuu ya kutaka mabadiliko katika nyanja mbali mbali.
Serikali ya awamu ya nne ilionekana dhaifu katika utendaji na utoaji wa maamuzi.
Pale ilipotokea kashfa au mgogoro unaohusu serikali, ziliundwa tume mbali mbali kwa ajili ya kutafuta chanzo cha mgogoro na njia ya kutatua huo mgogoro.
Utaratibu huu ulilalamikiwa na wapinzani kwani walituaminisha wananchi kuwa huko kuunda tume ni uootevu wa rasilimali pesa na muda kwani maamuzi yangeweza kufanywa bila ya kuundwa kwa tume (maamuzi ya papo kwa papo).
Awamu ya tano ilipoingia madarakani ikaamua kulifanyia kazi hilo suala kwa viongozi kutoa maamuzi ya hapo kwa hapo (Doh! wapinzani wanatuambia serikali ya kukurupuka).
Uongozi wa awamu ya nne uliamua kukaa kimya kuhusu kuwataja wapiga dili wa ngada (Tuliambiwa jamaa ni dhaifu).
Ilipoingia awamu ya tano amejitolea kijana kuwataja wanaosadikiwa kutumia au kujihusisha na ngada katika awamu ya kwanza ya waliotajwa, wakajitokeza watu na kupinga wakidai kuwa waliotajwa ni vidagaa tu mapapa hawawezi kutajwa.
Awamu ya pili ikaibuka na majina ya watu wazito katika jamii.
Kilichifuata tukaambiwa kwanza huyo anaetaja wenzake amelipwa na cartel zingine za wauza ngada ili kuchafua au kuharibu biashara za wengine, walipoona haina uzito sasa wamegeukia kumuandama mtaja wenzake kwa kuulizia utajiri wake na pia kuhus elimu yake.
Na zaidi wanapokea wale waliosaidia chama cha kijani kushika nchi tena wanawasaidia katika kesi zao.
Kwa kuhitimisha Kikwete alikuwa sawa kukaa kimya na kuendesha nchi anavyoona yeye inafaa na si kwa kusikiliza watu wanasemaje, kuna wakati alitoka nje ya nchi na aliporudi nchini kufika pale airport aliulizwa swali na mwandishi watu wengi wanalalamika kuwa safari zake hazina tija, kama kawaida ya mkwere tabasam pana akamjibu mwandishi nanukuu "unapoishi katika jamii kuna15% ya watu hata ufanye ubaya gani watakupenda tu, kuna 15% ya watu watakuchukia hata ufanye jema lipi wenyewe watakuchukia tu na 70%"ya watu waliobaki hawa ni bendera kufuata upepo"
Nawasilisha!!!