Kikwete akemee wahisani

Inkoskazi

Member
Apr 12, 2010
33
15
Tulimshuhudia Kikwete akiwakaripia wafanyakazi (TUCTA) pamoja na vitisho vingi dhidi yao na kuhitimisha kwamba hazihitaji kura zao (kama vile tayari ameshachaguliwa kuwa mgombea wa urais na chama chake).
Majuzi tumewasikia wahisani nao wakisitisha kuchangia katika bajeti yetu, ingekuwa vizuri Kikwete akawaita tena "wazee wa CCM - D'salaam)" akawahutubia na kuwakaripia na kuwatisha wahisani kuwa atafunga balozi zao na ahitimishe kwamba hahitaji pesa zao waondoke na atakayekaidi vyombo vya dola vitamshughulikia.



"Moringe wote ni wamasai lakini sio kila mmasai ni Moringe"
 
Nakuunga mkono ndugu yangu mmasai, kama kweli yeye ni kiongozi makini afanye hivyo, nawapongeza pia wahisani kwa hatua yao ya kutusaidia kupunguza pengo kati ya wakina kikwete na sisi watu wakawaida, labda safari za bwana mkubwa zitapungua ili walau watu wake nao wajue ugumu wa maisha yetu watanzania. HUREE WAHISANI
 
Awakemee Wahisani?

Tangu Lini Matonya akamkemea yule anayemdondoshea chenji kwenye bakuri lake?
 
Back
Top Bottom