Kikundi cha IS chauwa wanajeshi 32 wa Libya

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Wanajeshi 32 wa serikali ya Libya wameuawa katika makabiliano na wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS na katika mripuko wa gari uliosababishwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga karibu na mji wa Sirte.

Hayo yamethibitishwa na jeshi la serikali, na kitengo cha operesheni kilichoundwa na serikali mpya ya umoja wa kitaifa ya Libya. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, kitengo hicho kimesema watu wengine 50 wamejeruhiwa.

Taarifa zilizofuata zilieleza kuwa wanajeshi wa serikali walikuwa wakisonga mbele dhidi ya wanamgambo wa IS, na kwamba wameweza kuikomboa miji mitatu karibu ya Sirte, ambao ni ngome kuu ya IS nchini Libya.

Miji hiyo iliyokuwa imekamatwa na IS mapema mwezi huu, imetajwa kuwa Abugrein, al-Washka na Wadi Zamzam, hii ikiwa ni kulingana na ripoti ya shirika la habari la DPA, likikariri taarifa ya shirika la habari la Libya, LANA.

Chanzo: DW
 
Hayo mashetani si ya kuyakamata. Ni kuyatikita moja kwa moja kwa sababu si binadamu tena na hakuna lugha yoyote ya kibinadamu yanaelewa zaidi ya ile ya shetwani baba lao na muungu lao.
 
Hayo mashetani si ya kuyakamata. Ni kuyatikita moja kwa moja kwa sababu si binadamu tena na hakuna lugha yoyote ya kibinadamu yanaelewa zaidi ya ile ya shetwani baba lao na muungu lao.
hiyo ndo demokrasia waliyokuwa wanaililia wananchi wa libya, MAREKANI MJANJA SANA.
 
Back
Top Bottom